Kocha Robert Matano aondoka Tusker FC baada ya mkataba kuisha

Matano alijiunga na Tusker fc 2018 baada ya kuondoka katika Afc leopards.

Muhtasari

•Kocha Robert Matano ameondoka Tusker FC baada ya kandarasi yake kukamilika na wanamvinyo hao.

•Matano ameshinda mataji mawili ya ligi kuu ya fkf na wanamvinyo Tusker  Fc 2020-21,2021-2022 tangu 2018.

Robert Matano
Image: Facebook

Kocha mkuu wa Tusker FC inayoshiriki ligi kuu ya fkf,Robert Matano ameondoka baada ya kandarasi yake kukamilika.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 ,alijiunga na wanamvinyo Tusker Fc mwaka wa 2018 huku akishinda mataji mawili ya ligi kuu ya fkf pamoja na kushinda kocha bora wa mwezi Juni 2021 na kocha bora wa msimu 2020/21.

Matano amekuwa miongoni mwa wakufunzi wenye uweledi  hapa nchini akiwa amenoa baadhi ya vilabu kama vile Afc Leopards mwaka 2017, Ulinzi Stars 2024-2016  World Hope fc 2005-2007. Matano alishinda taji la fkf na Sofapaka mwaka wa 2009,

Jinsi wengi wanvyomfahamu kama 'Lion' anatambulika kwa 'tactic ' zake huku akisalia kuwa kocha ambaye ameshinda mataji mengi ya fkf kuliko kocha yoyote kutoka hapa nchini.

Baadhi ya vilabu vitakuwa mbioni sasa kutafuta huduma zake hasa wakati huu ambao hana klabu. Kwa miaka sita ambayo amekuwa Tusker fc ,Matano hajawahi maliza nje ya timu nne bora kwenye ligi ya fkf.