logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Thiago silva aiongoza Fluminense kutofungwa kwa mara ya kwanza katika mechi 11

Thiago Silva alicheza mechi yake ya kwanza tangu kujiunga na Fluminense baada ya kandarasi yake ya Chelsea  kukamilika.

image
na Davis Ojiambo

Michezo22 July 2024 - 08:15

Muhtasari


  • •Thiago Silva alicheza mechi yake ya kwanza tangu kujiunga na Fluminense baada ya kandarasi yake ya Chelsea  kukamilika.
  • •Fluminense iliipiga Cuiaba 1-0 kwenye mechi ya ligi kuu ya Serie B kule Brazil

Klabu inayoshiriki ligi kuu ya Brazil, Fluminense ilifanikisha kuzuia kutofungwa kwa mara ya kwanza baada ya mechi 11.

Hii ni baada ya beki wa zamani wa Chelsea, Thiago Silva kuongoza safu ya ulinzi kwenye mechi yake ya kwanza na klabu hio.

Kwenye mechi  11 za awali  walizokuwa wakicheza, Flumimense hawakuwa wameweka 'cleansheet' yoyote ile. Kwa sasa wanashikilia nafasi ya 19 kwenye jedwali mbele ya Atletico Go, wanaoburura mkia.

Ushindi wa Julai 21,2024 dhidi ya Cuiaba ulikuwa wa pili kwa klabu hio ya Brazil tangu Aprili 20,2024 kwenye ligi kuu ya Brazil ambapo waliwapiga Vasco da Gama 2-1 .

Silva alionyesha kufurahia baada ya mchezo huo huku akisema;

"Ni miaka 16 tangu nijawe na hisia nzuri kiasi hiki kuvaa jezi hii uwanjani. Bila shaka, huu ni muda ambao sitaweza kusahau na namshukuru Mungu kwa kuwa pamoja nami na kutusaidia kupata ushindi usiku huu." Silva alisema.

Silva alicheza kwa mara ya kwanza  licha ya kujiunga na klabu hio  mnamo Mei kwa kuwa dirisha la uhamisho nchini Brazil lilifunguliwa rasmi Julai 10.

Kifungu cha 10 cha kanuni mahususi za kitengo cha kwanza cha Brazil kinasema kwamba mchezaji mpya anaweza kuanza kushiriki mashindano siku moja baada ya jina lake kuchapishwa.

Silva ,39 aliondoka Chelsea Mei baada ya kandarasi yake kukamilika.Ameichezea klabu hiyo mara 152 na kusaidia kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya   mwaka 2021.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved