Manchester united wazindua jezi mpya ya ugenini msimu 24/25

Jezi hii inaleta urejesho wa miaka ya awali

Muhtasari

•Manchester United wamezindua jezi yao mpya ya ugenini kwa msimu ujao 2024/25

•Jezi hii inaleta urejesho wa aina ya miundo ambayo United ilikuwa ikivaa miaka ya 1990.


Jezi mpya ya ugenini ya Manchester united Picha: Manchester united
Image: Manchester united

Klabu ya Manchester United imezindua jezi mpya ya ugenini kwa msimu ujao wa 2024/25.

Msingi wa rangi ya  'navy blue 'unaonyesha  msururu wa ruwaza za duara katika kivuli tofauti cha samawati kote na umechorwa kama urejesho wa aina ya miundo ambayo United ilikuwa ikivaa miaka ya 1990.

Pamoja na kuenzi historia ya klabu, muundo huo pia unalipa heshima kwa jiji la Manchester. Vivuli vitatu vyepesi vya rangi ya samawati vimepita kwenye kola kama marejeleo ya mito mitatu ya jiji - Irk, Medlock na Irwell. Maelezo ya adidas yanaonekana kwa rangi ya fedha.

Jezi hiyo pia ina nembo ya Snapdragon kampuni inapoanza mwaka wake wa kwanza kama mfadhili wa jezi za msingi za United. Kampuni ya teknolojia ya Marekani inachukua nafasi ya TeamViewer iliyokuwepo msimu uliopita.

Baaadhi ya mashabiki wameonyesha hisia mseto kuhusu jezi hiyo mpya kupitia mitandao ya kijamii huku wengi wakisifia na baadhi kukashifu.

Vile vile, Manchester United walithibitisha kuwa mshambulizi  Rasmus Hojlund  atavalia jezi namba 9 kufuatia  kuondoka kwa Anthony Martial.

Raia huyo kutoka Denmark alivaa nambari 11 katika kampeni yake ya kwanza na  wekundu  hao wa Manchester,nambari ambayo ilihusishwa zaidi na mawinga wakubwa wa miaka iliyopita.

United wanatazamiwa kumenyana na Arsenal Jumapili ya Julai 28,mechi ya kirafiki,kwenye Uwanja wa SoFi huko Los Angeles, kabla ya kumenyana na Real Betis huko San Diego Alhamisi 1 Agosti  na Liverpool huko South Carolina. Jumapili 4 Agosti.