•Chelsea imewasajili wengine kadhaa msimuu huu w wakiwemo Tosin Adarabioyo, Estevao Willian, Omari Kellyman, Filip Jorgensen, Marc Guiu na Kiernan Dewsbury-Hall.
Chelsea wamekamilisha usajili wa beki wa Boca Juniors Aaron Anselmino kwa mkataba wa pauni milioni 15.6.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 amesaini mkataba wa miaka saba Stamford Bridge lakini atasalia kwa mkopo katika klabu hiyo ya Argentina msimu wa 2024-25 kama sehemu ya makubaliano hayo.
Alianza kucheza Boca mnamo Juni 2023 na amecheza jumla ya mechi 10.
Anselmino alitia saini nyongeza ya kandarasi mnamo Januari 2024 ambayo ilimfunga kwa kilabu hadi 2028.
Chelsea imewasajili wachezaji wengine kadhaa msimuu huu wa joto wakiwemo Tosin Adarabioyo, Estevao Willian, Omari Kellyman, Filip Jorgensen, Marc Guiu na Kiernan Dewsbury-Hall.
Takriban pauni milioni 90 zimerupatikana kupitia mauzo ya Ian Maatsen, Lewis Hall na Omari Hutchinson huku Conor Gallagher akitarajiwa kujiunga na Atletico Madrid.
The Blues wako sokoni kutafuta mshambuliaji na wanamtaka mshambuliaji wa Atletico Madrid, Samu Omorodion.
Chelsea wataanza watafungua mechi ya Ligi Kuu ya 2024-25 dhidi ya mabingwa Manchester City mnamo Agosti 18.