Nahodha wa Harambee Starlets U20 Jane Hato yuko salama

Timu ya kandanda ya wanawake inayoshiriki ligi kuu ya wanawake umu nchni, imetoa taarifa kuhusiana na kupotea kwake mchezaji Jane Hato.

Muhtasari

•Shirikisho la soka nchini FKF nchini siku ya Alhamisi lilikuwa limeripoti kutoweka kwake, lakni sasa inasemekana amepatikana  na ataunganishwa na familia yake. 

JANE HATO
JANE HATO
Image: JANE HATO//FKF

Nahodha wa timu ya kinadada ya Kenya isiyozidi umri nwa miaka 20 na kenya police Bullets Jane Hato yuko salama.

Shirikisho la soka nchini FKF nchini siku ya Alhamisi lilikuwa limeripoti kutoweka kwake, lakni sasa inasemekana amepatikana  na ataunganishwa na familia yake. 

Chris Oguso afisa mkuu mtendaji wa Kenya Police Bullets alisema kwamba Hato yuko salama na walitumia kila mbinu kuhakisha kwamba wamepata taarifa kuhusiana na kupotea kwake. 

"Sidhani kama haya ni maswala yanayofungamana na kandanda ila huenda ikawa ni mgogoro wa kifamilia ,na washikadau wetu wanazidi kutatua chanzo cha kupotea,mahali aliko na mtu ambaye wako naye,na pindi tu watasuluhisha, atajiunga na kikosi ambacho kimesafiri Ethiopia " Oguso alisema .

Aidha Oguso alisema kuwa kutokana na udukuzi wao, Hato yupo na mtu anayemjua. Hato alitarajiwa kukiongoza  kikosi cha timu hiyo ya Bullets ,katika michuano ya kujikatia tiketi kucheza kwenye CAF champions league , Ethiopia.

Aidha kutoweka kwake ni jambo ambalo liliwapa familia na marafiki  wake kipindi kigumu huku wakitoa ombi kupiga ripoti kwa atakaye muona.