West Ham yapata nahodha mpya, Jarrod Bowen

Winga matata wa timu ya West Ham United na timu ya Taifa Ya Uingereza Jarrod Bowen ametwikwa jukumu la kuia nahodha mpya wa timu hiyo.

Muhtasari

• Jarrod Bowen achaguliwa kuwa nahodha mpya wa klabu ya West Ham United kabala ya msimu kuanza baada ya Kourt Zouma aliyekua nahodha hapo awali kuhamia klabu ya uharabuni.

JARROD BOWEN
JARROD BOWEN
Image: JARROD BOWEN//WEST HARM UNITED

Kocha wa klabu ya West Harm united  inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza Julen Lopetegui sasa amemteua Jarrod Bowen kama nahodha mpya wa timu hiyo msimu huu mpya.

Bowen atakuwa akiridhi mikoba ya unahodha kutoka kwa aliyekuwa beki wa Chelsea Kourt Zouma baada ya kuhamia klabu ya Shabab ya uarabuni.

Bowen amekua mwiba katika safu ya uvamizi na kusaidia timu hiyo kutwaa taji la UEFA conference league  mwaka wa 2023. Mzawa huyo wa Uingereza anatarajiwa kutamba sana wakati ligi kuu nchni humo inatarajiwa kuanza .Aidha, Bowen alifanya vyema katika kipute hicho na kuwa mchezaji bora katika mechi ya fainali ,vilevile ,mchezaji bora wa kipute hicho makala yaliyopita.

Bowen anadhihirisha uwezo wake baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha  Uingereza kilichocheza kwenye makala ya yaliyopita ya Euro Ujerumani huku Taifa hilo likifika katika fainali na kulemewa na vijana wa Uhispania.

West Harm United ilifanikiwa kumaliza nafasi ya 14 msimu jana licha kusuasua na kupokea vipigo vya magoli mengi katika msimu huo,klabu hiyo sasa imejipanga vyema kwa msimu huja baada ya kufanya usajili wa majina tajika akiwemo mshambuliaji Fullkrug na beki Wan Bissaka kutoka Man United.