Ilkay Gündogan arejea Man City baada ya kuondoka msimu mmoja uliopita

Baada ya kuondoka kwenda klabu ya Barcelona,Gündogan amerejea klabu ya Man City chini ya ukufunzi wake Pep Guardiola.

Muhtasari

•Ilkay Gündogan amerejea katika timu ya Manchester City kama mchezaji huru kutoka katika timu ya Barcelona inayoshiriki katika ligi ya La Liga nchni Uhispania.

• Kiungo huyo ataichezea mabingwa hao hadi mwaka kesho ambapo atakua huru kuongeza msimu mmoja.

ILKAY GUNDOGAN
ILKAY GUNDOGAN
Image: ILKAY GUNDOGAN//FACEBOOK

Kiungo mshambulizi Ilkay Gündogan amerejea katika klabu ya Manchester City, baada ya kcheza  katika klabu ya Fc Barcelona inayoshiriki katika ligi kuu ya Uhispania, La Liga.

Gündogana aliichezea timu ya Man City na kuisaidia kunyakua mataji tajika katika ligi ya premia na barani Ulaya.

Kocha wa Man City ,Pep amesema kwamba amekubali ombi la Gündogan kurejea katika klabu hiyo hadi mwaka ujao wa 2025 na mazungumzo ya kuongeza msimu mmoja yakiwa huru.

Gündogan ameondoka katika klabu hiyo ya Barcelona kama mchezaji huru.

Aidha,mchezaji huyo alicheka na nyavu  mara 5 na kuwa katika nafasi ya saba wachezaji waliofunga mabao mengi katika klabu hiyo.

Gündogan,anatarajiwa kuisaidia mabingwa hao mara nane wa ligi kuu Uingereza katika kutetea taji lao msimu huu baada ya kuanza vizuri kwa kuibamiza timu ya Chelsea mabao mawili kavu ugenini.

Vile vile,Kocha mkuu wa City Pep,amefurahishwa na uamuzi wa Gündogan kurejea Man city na yuko sawa kujumuishwa katika mechi ifuatayo ambapo timu hiyo itacheza na klabu Ipswich Town waliopandishwa ngazi msimu huu.