Mshambuliaji wa Chelsea, Armando Broja kuelekea Ipswich Town kwa mkopo

Ipswich watagharamia mshahara wa Broja na kuna kipengele cha kumnunua kabisa kutoka Chelsea ikiwa mshambuliaji huyo atawasaidia kusalia kwenye ligi kuu ya premia msimu ujao.

Muhtasari

• Ujio wa kocha mpya, Enzo Maresca umeonyesha dalili kwamba mchezaji huyo hana lake tena katika kikosi cha Chelsea msimu huu na chaguo bora kwake ni kukipipiga kibarua chake kwingine.

ARMANDO BROJA
ARMANDO BROJA
Image: ARMANDO BROJA//FACEBOOK

Timu ya Ipswich Town,iliyopandishwa ngazi msimu huu ,imekubaliana na klabu ya Chelsea kumchukua mshambuliaji Armando Broja, ambaye atajiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mzima.

Aidha Chelsea,wameiambia timu ya Ipswich, kwamba ni lazima wamsajili Broja kwa mkataba wa kudumu endapo atawasaidia kutoshushwa daraja mwishoni mwa msimu huu,kwa kima cha £30m.

Ipswich ilimaliza katika nafasi ya pili katika ligi ya daraja la pili kwa alama 96 ,sasa wako kwenye mchakato wa kuwania ligi licha ya kuchabangwa mabao mawili kavu na timu ya Liverpool katika uga wa nyumbani.

Armando Broja amekuwa mchezaji mwiba hasa kutafuta mabao pale The Blues lakini hajaweza kupata nafasi ya kucheza katika michuano mingi.

Ujio wa kocha mpya, Enzo Maresca umeonyesha dalili kwamba mchezaji huyo hana lake tena katika kikosi cha Chelsea msimu huu na chaguo bora kwake ni kukipipiga kibarua chake kwingine.

Broja ambaye alizaliwa Uingereza ,lakini anaitumikia timu ya taifa ya Albania, anauzoefu baada yakuwa amejumuishwa katika klabu hiyo na kupata tajiriba .Kinda huyo ambaye alitokea klabu ya BurnHam, amezichezea klabu za FulHam united na Southampton kwa mkopo na kuchangia pakubwa katika timu hizo.

Kuondoka kwake pale Chelsea kumechamngiwa pakubwa mna sajili ambazo timu hiyo inafanya, na kwaivyo kukosa nafasi.

Broja anatarajiwa kutamatisha vipimo vyake vya kiafya kabla ya leo,katika timu hiyo chini ya mkufunzi Kieran Mckenna ambaye aliwaziwa kuchukua pengo lake Pochettino.