Amos Wanjala ajiunga na klabu ya Athletic Club Torrellano

Wanjala ambaye aliibuka kutoka na umahiri wake katika michuano ya shule za upili huku akiichezea St Antony,Kitale.

Muhtasari

•Kinda kutoka Kenya Amos wanjala ajiunga na timu inayoshiriki katika daraja la 5 kwenye ligi ya Uhispania AC Torrellano ili kutoa huduma zake .

•Wanjala ambaye aliibuka kutoka na umahiri wake katika michuano ya shule za upili huku akiichezea St Antony,Kitale.

•Wanjala amekuwa hodari kutokana na yeye kukiongoza kikosi kilichomaliza nafasi ya pili kwenye mashindano ya CECAFA yaliokuwa yameandaliwa disemba mwaka jana ,Kisumu.

AMOS WANJALA BAADA YA MECHI YA CECAFA U18
AMOS WANJALA BAADA YA MECHI YA CECAFA U18
Image: AMOS WANJALA//FACEBOOK

Beki wa Kenya Amos Wanjala anayeimarika kwa kasi mno,amejiunga na klabu  Athletic Club Torrellano,inayoshiriki ligi ya daraja la tano nchni Uhispania.

Wanjala ,umaarufu wake umechangiwa pakubwa na kuhamia kwake nchni Uhispania alipokuwa amejumuika na wenzake ,ikiwemo Aldrine Kibet na Alvin Kasavuli miongoni mwa makinda wengine kutoka Kenya ,wanaosakata kandanda.

Watatu hao,walijiunga na akademia ya Nastic sports,kutokana na wao kuonyesha mchezo wa kupendeza hasa katuka michuano ya shule za upili ,wakichezea timu ya wavulana ya St Antony Kitale.

Wanjala,aidha,aliisaidia timu hiyo ya St Antony kutwaa taji hilo la shule za upili,huku akiwa nguzo kubwa na kuwa katika nyoyo za mashabiki hususan wa timu hiyo.Aidha,Wanjala ,aliongoza kikosi cha Taifa katika michuano wa CECAFA cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 mjini Kisumu na kumaliza katika nafasi ya pili.

Wanjala ambaye ameonyesha uhodari wake kama mlinzi wakati ,lakini kwa sasa anacheza nafasi tofaui ikiwemo kama kiungo mkabaji akichezea timu hiyo a Athletic .

Timu hiyo ya Ac Torrellano amabyo ilianzishwa mwaka wa 2012 na uchezea katika uga wao wa Campo Municipal Isabel Stadium.