Chelsea yasaka huduma zake Ivan Toney

Klabu ya Chelsea sasa imefungua mazungumzo na klabu ya Brentford kuhusiana na usajili weke Ivan Toney

Muhtasari

•Klabu ya Chelsea imeanza mazungumzo na timu ya Brentford ili kumsajiliu mshambuliaji Ivan Toney kabla ya dirisha la uhamisho kufikia ukingoni na ligi kuu humo kushika kasi ikiingia wiki ya tatu ijumaa hii.

Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY

Klabu ya Chelsea sasa imefungua mazungumzo na klabu ya Brentford kuhusiana na uwezekano wa  kumsajili Ivan Toney.

The Blues wanachukua hatua hiyo baada ya usajili wake mshambuliaji wa timu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu ya Italia Victor Osimhen kugonga mwamba.

Chelsea bado wako tayari kutafuta mshambuliaji ambaye atachangia pakubwa katika utafutaji wa mabao klabuni humo,na pendekezo kubwa ni mshambulizi huyo ambaye amedhihirisha uwezo wake akichezea Brentford na timu ya Taifa la Uingereza.

Toney,licha ya kupigwa marufuku baada ya kupatikana na hatia ya kucheza kamari katika soka,na kukaa nje kwa kipindi kirefu,ameonekana bado yuko na makali ya kutosha na sasa Chelsea wako tayari kumsajili.

The Blues ,wamekuwa wakifukuzia mchezaji wa Napoli Victor Osihmen,na ambaye kwa sasa kulingana na muonekano wa mambo,huenda asijiunge na klabu hiyo kutokana na kutokuepo kwa mazungumzo bayana baina ya klabu ya Chelsea na agenti wake.

Chelsea wanawania huduma za mchezaji huyo ambaye vile vile anawindwa na klabu kutoka Uarabuni.

Duru za kuaminika zinaashiria kuwa ,mazungumzo yameanza baina ya vilabu vyote viwili ili kuona kuwa Ivan Toney,anmajiunga na Chelsea ,iwapo mazungumzo yenye matunda na makubaliano yatafanyika kabla ya dirisha uhamisho likikaribia.

Chelsea wameonekana kuamka baada ya ushindi dhidi ya Wolveha

Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY
Image: INSTAGRAM// IVAN TONEY