• ‘Sio Raheem pekee. Ni wachezaji wote ambao kwa wakati huu wanafanya mazoezi mbali. Wakati dirisha la uhamisho linafungwa, hawatapata dakika.’
Mkufunzi wa Chelsea Enzo Maresca anasisitiza Raheem Sterling na wachezaji wengine wa kikosi chake 'hawatapata dakika YOYOTE' ikiwa watashindwa kupata pa kutoka kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama.
Katika pambano lisilo la kawaida lililotupwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 29 na wengine wanaofanya mazoezi mbali na kikosi chake cha kwanza akiwemo Ben Chilwell na Trevoh Chalobah, Maresca alieleza hawatopata hata sekunde kuchezea Chelsea.
Akizungumza na vyombo vya habari mjini Geneva kabla ya kumenyana na Servette kwenye Ligi ya Konferensi siku ya Alhamisi, kocha mkuu wa Chelsea alisema kuhusu Sterling: ‘Ushauri wangu. Anajua hasa anachopaswa kufanya. Hahitaji ushauri wangu. Tunakwenda kuona.”
'Napendelea kuwa mkweli kwa mchezaji. Wale ambao hawajahusika, wote ni wachezaji ambao hawatahusika na hawapati dakika yoyote endapo watabaki.”
‘Tutaona ni nani aliye hapa na nani hayupo hapa. Kitu pekee ninachoweza kusema ni wale ambao watapata dakika ni wale ambao nadhani wanaweza kutusaidia.
‘Sio Raheem pekee. Ni wachezaji wote ambao kwa wakati huu wanafanya mazoezi mbali. Wakati dirisha la uhamisho linafungwa, hawatapata dakika.’
Vyanzo vya karibu na Sterling vinasema kuwa hawatalazimishwa kufanya hatua ambayo haiwafai, na kuongeza kuwa kuna nafasi nyingi za yeye kusalia kama ilivyo.
Maresca pia aliulizwa kuhusu Jadon Sancho wa Manchester United, ambaye anaweza kutengeneza nusu ya mpango wa kubadilishana na Sterling kabla ya dirisha kufungwa.
Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 44 alisema Chelsea haitasajili mchezaji kwa ajili yake lakini aliongeza alipoulizwa Sancho: ‘Ikiwa tunaweza kusajili mchezaji ambaye anaweza kutusaidia, kwa hakika nataka. Namjua sana Jadon. Lakini yeye si mchezaji wetu. Tutaona kitakachotokea.’