Droo ya Champions League yafanyika

Timu 36 ,zitashiriki katika kombe la Champions League ,huku Real Madrid wakiwa mabingwa watetezi

Muhtasari

•Kombe la Maskio marefu ulimwenguni (champions League) larejea huku timu 36 zikipata nafasi ya kushiki ambapo timu nne kutoka ligi moja zitapata nafasi ya kushiriki kando na apo awali timu tatu zikishiriki kutoka ligi moja.

•Mfumo wa kidijitali kutumika katika kupanga na kuchagua mechi za makundi ambapo timu zote zipo katika vyungu vinne.

•Timu zote kuwekwa katika vyungu vinne,na kushiriki mechi nane katika hatua za makundi.

•Mechi hizo zitang'oa nanga mnamo septemba 14,2024.

champions league pots
champions league pots
Image: hisani

Baada ya ligi kuu katifa mataifa tofauti tofauti kutamatika msimu uliopita na timu kupata fursa ya kushiriki katika kombe la maskio marefu,Champions League,sasa orodha ya michuano itakayo jumuisha timu 36, imetoka ,hii ni kufuatia droo iliyofanyika usiku wa alhamisi.

Timu  za kutoka  ligi kuu ya Uingereza ambapo ni timu ya Manchester City, Arsenal, Aston Villa na timu ya Liverpool sasa zitawania taji hilo angalau kulirejesha Uingereza huku timu ya Man Cityb ikiwa timu ya mwisho kutoka ligi hiyo kubeba taji hilo mwaka wa 2022/23 walipo ipiga timu ya Inter Milan bao moja sifuri.

Aidha,ni orodha ambayo inautata mwingi baada ya kamati andalizi UEFA,kutumia mfumo tofauti kando na apo awali na kutoa mageuzi yafuatayo.

  • Timu 36 kushiriki katika michuano hii.
  • Timu 4 kutoka ligi moja kupata nafasi kushiriki.
  • Timu kucheza michuano minane katika hatua ya makundi na timu tofauti kando na timu 3 awali.
  • Mabingwa wa ligi, watakuwa katika chungu cha kwanza kati ya vyungu vinne kulingana na nafasi timu ilimaliza katika ligi.
  • Kila timu itamenyana na timu mbili kutoka kila chungu .
  • Timu kutoka ligi moja hazitapatana na zitajumuishwa kwa chini ya makundi mawili yenye timu zinazoshiriki ligi moja.
  • Mfumo wa kidijitali kutumika katika kuchagua timu katika vikundi kamdo na hapo awali.
  • Zaidi ya mipira ya soka 1000 kutuimika katika hatua ya makundi .

Mfumo huu ambao ni  wa kidijitali ,utarahisisha kuchagua timu na kuwa na ukosefu wa kupendelea timu katika ugombeaji dhidi ya wapinzani.Timu zote 36 ziko katika vyungu vinne.

Michuano ya makundi inaratibiwa kuchezwa kati ya tarehe 14-15 ,septemba, 2024.

 

champions league pots
champions league pots
Image: hisani