Noni Madueke ajumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza kwa mara ya kwanza

Winga na mshambuliaji matata wa timu ya Chelsea sasa amepata mwaliko wake wa kwanza kwa timu ya taifa ya Uingereza ya wakubwa.

Muhtasari

•Winga wa klabu ya Chelsea matata, Noni Madueke, sasa amejumuishwa katika timu ya Taifa ya Uingereza ambapo taifa hilo linatarajiwa kumenyana na Ireland na Finland katika European Nations League.

•Kipute hicho kinatarajiwa kuanzia wakatiti ligi zitakwenda mapumuzikoni,septemba na fainali kuchezwa juni 2025.

•Harry Maguire,,Angle Gomes na Jack Grealish pia wao wamerejea kikosini.

•Timu hiyo ya Uingereza itacheza chini ya ukufunzi wake kocha mpya ,Lee Carsley,aliyeridhi mikoba yake Gareth Southgate aliyejiuzulu kama kocha baada ya msururu wa matokeo mabovu na kukosa kushinda taji.

ENGLAND //2024 NATIONS LEAGUE SQUAD
Image: HISANI

Mchezaji wa klabu ya Chelsea Noni Madueke sasa ameweza kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Uingereza kwa michuano ya kipute cha Nations League dhidi ya Taifa la Ireland na Finland.

Hii ni baada ya  Uingereza kumpiga kalamu kocha Gareth Southgate ambaye aliacha kazi baada ya shinikizo kutokana na ukosefu wa kutoshinda mataji.

Lee Carsley,ambaye aliiridhi mikoba yake Southgate,sasa amekitaja kikosi hicho ambacho kitashiriki michuano ya Nations League ambayo inatarajiwa kuchezwa kuanzia septemba,na hatimaye fainali kuchezwa Juni 2025.

Baadhi ya wachezaji ambao vile vile wamejumuishwa katika kikosi ni pamoja na Harry Maguire,Angle Gomes na Jack Grealish.

Madueke ambaye amekuwa akicheza katika timu ya taifa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 na katika michuano ya kutafuta nafasi ya kushiriki European Championship 2025,alifunga mabao sita kati ya mechi saba alizocheza.

Madueke mchango wake mkubwa kujumuishwa kikosini umejiri juma moja tu baada ya kufungia Chelsea mabao matatu katika mechi ya  ligi kuu nchini UIingereza wakati klabu hiyo ilipolaza Wolveharmpton mabao 6-2.

Madueke,amekuwa mwiba hasa katika ufungaji mabao na anajulikana sana kwa chenga zake za maudhi.