Kylian Mbappè afungua akaunti yake ya mabao katika ligi ya La Liga

Real Madrid sasa wanatajia mshambulizi huyo kutoa huduma zake sio tu katika ligi bali pia kwenye kombe la mabingwa huku wakiwa mabingwa watetezi.

Muhtasari

•Kylian Mbappè aMEanza kuonyesha ubora wake katika klabu ya Real Madrid ambapo ni msimu wake wa kwanza baada ya kusajiliwa kutoka PSG ya Ufaransa.

•Mshambulizi huyo alicheka na nyavu wakati klabu hiyo ilkuwa inamenyana na klabu ya Real Betis na kufunga mabao mawili ya muhimu,ili kutia pointi tatu mfukoni.

KYLIAN MBAPPE
Image: REAL MADRID//FACEBBOK

Mshambuliaji wa taifa la Ufaransa anayechezea timu ya Real Madrid inayoshiriki katika ligi kuu ya Uhispania,La Liga, Kylian Mbappè ameanza kutoa kucha zake ya makali baada ya kuchana nyavu mara mbili wakati klabu ya Real Madrid ilimenyana na klabu ya Real Betis.

Mbappè aliisaidia timu hiyo kupata ushindi wa mabao mawili kwa sufuri na kuweka matumaini yao ya kuwania taji ligini humo baada ya kuanza kwa kusuasua.

Mbappè ambaye alisajiliwa kutoka klabu ya PSG,na kukubalika sana na mashabiki wengi duniani hasa katika fani ya kandanda,amekuwa mwiba hasa anapopiga mikimbio na chenga za maudhi katika eneo la hatari la wapinzani.

Mbappè ambaye alianza taaluma yake ya soka katika klabu ya Ac Monaco ya Ufaransa na hatimaye kujenga taaluma yake kikamilifu pale PSG na kuwasaidia kupata mataji sii haba akiwa huko kama vile taji la ligi kuu ya ufaransa League 1.

Real Madrid sasa wanatajia mshambulizi huyo kutoa huduma zake sio tu katika ligi bali pia kwenye kombe la mabingwa huku wakiwa mabingwa watetezi.