Luis Suárez astaafu soka ya kimataifa

Luis Suarez ametundika daluga zake kucheza katika kandanda ya kitaifa akiwa na umri wa miaka 37 ,kwa sasa akichezea timu ya Inter Miami,inayoshiriki ligi ya MLS

Muhtasari

•Luis Suárez amesema kuwa amestaafu kucheza katika kandanda ya kimataifa baada ya jumla ya mechi 142 huku akichana nyavu mara 69.

•Kwa sasa Suárez,anachezea timu ya Inter Miami,inayoshiriki ligi ya MLS,Amerika.

LUIS SUAREZ
Image: HISANI

Nyota wa Uruguay Luis Alberto Suárez Díaz ambaye amechezea taifa lake jumla ya mechi 142 ametangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa.

Suárez,ambaye ana umri wa miaka 37 amekuwa muhimu katika timu ya La Celeste.

Suárez kwa machozi amesema kuwa atacheza mechi yake ya mwisho ya timu hiyo ya La Celeste katika mechi za kujikatia tiketi kwa makala ya kombe la dunia 2026.

Mchezaji huyo wa Inter Miami,alichezea tima ya taifa ya Uruguay katika makala ya Copa America,na kucheza mechi ya kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Canada na hatimaye kumaliza katika nafasi hiyo baada ya mechi hiyo kuishia katika matuta ya penati.

Suárez,amekuwa mchezaji ambaye ana magoli mengi kwa mwonekano mara 142 huku akifunga mabao 69.

Suárez,wengi wanamkumbuka kwa kisa alichofanya cha kuzuia mpira kuingia wavuni na mikono yake wakicheza dhidi ya Ghana ,katika nafasi ya nusu fainali.Licha ya kupewa kadi nyekundu,mchezaji wa Ghana alishindwa kufunga penati na kwaivo timu hiyo ya Uruguay kupata nafasi ya kufika kwenye hatua za nusu fainali mara ya kwanza baada ya 1970.

Suárez ,aidha anakubukwa baada ya kumuuma beki Giorgio Chiellini beki wa timu ya Italy katika kombe la dunia 2014, Brazil.Hicho kilikua kisa cha tatu cheki baada yake kuwauma wachezaji Branislav Ivanovic na Otman Bakkal.

Kwa sasa Luis Suárez anaichezea timu ya Inter Miami ya Amerika inayoshiriki ligi ya MLS,na amekuwa mshambuliaji muhimu baada ya kujiunga na timu hiyo kucheza na Lionel Messi zamani wakicheza Barcelona.