C. Palace wasema lengo lao ni kufanya biashara na vilabu vikubwa baada ya Olise kuenda Bayern

“Tunajivunia ukweli kwamba Olise amekwenda Bayern. Tunataka kuuza kwa vilabu vya juu au vilabu vya juu ambao wana matarajio makubwa. Tunataka kucheza Ligi ya Mabingwa."

Muhtasari

• Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish alielezea fahari juu ya uhamisho wa Michael Olise kwenda Bayern Munich.

CRYSTAL PALACE.
CRYSTAL PALACE.
Image: FACEBOOK

Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish amefichua kwamba lengo lao ni kuendelea kufanya biashara za kuuza wachezaji na vilabu vikubwa vya soka si tu Uingereza pekee bali barani Ulaya kwa umla.

Akizungumza na runinga ya Sky Sports, Parish aliweka wazi kwamba kama klabu, wana furaha isiyo na kifani kwamba hatimaye walimuuza Michael Olise kwenda Bayern Munich ya Ujerumani.

Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish alielezea fahari juu ya uhamisho wa Michael Olise kwenda Bayern Munich.

Olise alijiunga na Bayern Munich kwa mkataba wa miaka mitano, unaoashiria hatua kubwa katika maisha yake ya soka. Crystal Palace inalenga kushindana katika viwango vya juu zaidi, ikiwa ni pamoja na Ligi ya Mabingwa.

Michael Olise alijiunga na Bayern Munich kwa mkataba wa miaka mitano hadi 2029. Ada ya uhamisho wa Olise inaripotiwa kuwa €60 milioni (£50.8 milioni) ikijumuisha nyongeza.

Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish alionyesha kufurahishwa na hatua ya Olise na kuangazia matarajio ya klabu.

“Tunajivunia ukweli kwamba Olise amekwenda Bayern. Tunataka kuuza kwa vilabu vya juu au vilabu vya juu kama Newcastle ambao wana matarajio makubwa. Tunataka kucheza Ligi ya Mabingwa. Ukweli ni kwamba hatufanyi hivyo kwa sasa", aliiambia Sky.

Michael Olise alihamia Crystal Palace kutoka Reading mwaka wa 2021. Ada ya uhamisho wa uhamisho huu iliripotiwa kuwa karibu £8 milioni.

Uchezaji wake katika Crystal Palace ulivutia vilabu kadhaa vya juu, vikiwemo Chelsea, Manchester United, na Newcastle United.