Cole Palmer aondolewa kwenye kikosi cha Uingereza

Kinda wa klabu ya Chelsea Cole Palmer ameondolewa kwa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachocheza katika michuiano ya Nations League.

Muhtasari

•Kinda wa timu ya Chelsea Cole Palmer,ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoshiriki michuano ya Nations League.

•Hili linakuja siku chache baada ya timu ya Three Lions,kumteua Lee Carsley kama kocha.

•Kwingineko,beki kulia wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa,pia yeye ameondolewa kikosini cha wachezaji wasio zidi u8mri wa miaka 21, baada ya kupata jeraha la mfupa wa paja.

COLE PALMER. MALO GUSTO
Image: HISANI

Klabu ya Chelsea,inayoshiriki ligi kuu Uingereza,imethibitisha kuondolewa kwa mchezaji wao mwiba Cole Palmer,kutoka kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.

Palmer alionekana kuwasaidia pakubwa vijana hao wa Uingereza katika kipute cha Euro,licha ya kucheza dakika finyu lakini alichangia pakubwa dakika alizocheza.

Wachezaji wengine ambao wameondolewa kikosini ni pamoja na mshambulizi wa timu ya Aston Villa Ollie Watkins na Phil Foden wa Manchester city.

Hatua hii inajiri siku chache baada ya kocha mpya Lee Carsley, kutoa orodha ya wachezaji ambao watakuwa wanashiriki katika michuano ya Nations League  tarehe 7 na 12 Septemba. Three Lions,watacheza  dhidi ya  Ireland na Finland. Wakati huu ligi zipo katika kipindi cha mapumziko.

Kisa cha kuondolewa kwa Palmer kikosini bado hakijawekwa wazi na mchezaji huyo wa The Blues,atakuwa mazoezini Cobham,kwa matayarisho ya mechi ya ligi kuu,dhidi ya AFC Bournemouth.

Kwingineko beki wa kulia,mzawa wa ufaransa  Malo Gusto vile vile ameondolewa kutoka  kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21, baada ya kupata jeraha la  paja wakati akiitumikia klabu yake ya Chelsea dhidi ya Crystal Palace.

Baadhi ya mashabiki wa Chelsea, wameonekana kufurahishwa na jambo hilo la Palmer kuondelewa katika kikosi hicho,wakisema itakuwa fursa nzuri yake kutopata jeraha na kujinoa vilivyo ili kumenyana na timu ya AFC Bournemouth wikendi ya tarehe 17 septemba 2024.