Kai Havertz wa Arsenal avunja rekodi mbaya ya miaka 7

Mshambuliaji wa Arsenali Raia wa Ujerumani Kai Havertz awa mchezaji wa kwanza kucheza dakika 90 na kutokuwa na pasi iliyokamilika baada ya misimu 7 ya ligi kuu Uingereza.

Muhtasari

•Kai Havertz amekuwa mchezaji wa kwanza baada ya misimu 7 ya ligi kuu Uingereza kucheza dakika 90 na kukosa kutoa pasi iliyokamilika.

•Havertz alicheza dakika zote wakati wa pambano la kuwania taji la EPL wakati walikuwa wanamenyana na mabingwa watetezi Man City.

Image: INSTAGRAM// KAI HAVERTZ

Mshambuliaji wa Arsenali Raia wa Ujerumani Kai Havertz amekuwa mchezaji wa kwanza kucheza dakika 90 na kutokuwa na pasi iliyokamilika baada ya misimu 7 ya ligi kuu Uingereza.

Havertz alicheza dakika zote wakati wa pambano la kuwania taji la EPL wakati walikuwa wanamenyana na mabingwa watetezi Man City katika uga wa Etihad na mechi hiyo kumalizika sare ya mabao 2-2.

Havertz, ambaye alisajiliwa kutoka klabu ya chelsea amekuwa akiisaidia timu hiyo ya Gunners katika shughli pevu ya kutafuta mabao tangia ajiunge nao, msimu uliopita.

Arsenali licha yakuwa na upungufu wa mchezaji mmoja baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mwisho wa kipindi cha kwanza.Leandro Trossard alionyeshwa kadi ya pili ya manjano na kupelekea vijana hao wa Mikel Arteta kucheza wakiwa wachezaji 10.

Arsenali kwa sasa musimu huu wanaongoza kwa timu ambazo zimepokea kadi nyekundu kwa mchezaji zaidi ya mmoja baada ya Declan Rice.

Aidha, kadi ya manjano ya pili iliyomsabibishia mchezaji huyo kadi nyekundu, wengi wameizungumzia kusema kuwa haikustahili kwa kuwa lilikuwa pambano lenye shinikizo si haba.

Kocha wa Arsenali Mikel Arteta alionekana kugadhabika sana na kufoka baada ya mchezaji huyo kuonyeshwa kadi nyekundu.

Kwa mchezaji Havertz,aliandikisha historia hiyo na kuonyesha kiwango cha chini cha mchezo wakati wa pambano hilo.