Junior Starlets kupimana nguvu na Ureno matayarisho ya FIFA

Timu ya Kenya ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 ilifuzu kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika hostoria.

Muhtasari

• Jumatano, Junior Starlets iliilaza Valencia mabao 4 kwa 1 kupitia Valarie Nekesa na Lindey Atieno waliofunga mabao mawili kila mmoja.

• Shindano la FIFA la wasichana wa chini wa umri 17 litaandaliwa nchini Jamhuri ya Dominican kuanzia Oktoba tarehe 16.

Mchezaji wa kikosi cha Junior Starlets katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ciudad Deportiva Del Valencia CF mnamo Jumatano 25,2024.
Valarie Nekesa Mchezaji wa kikosi cha Junior Starlets katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ciudad Deportiva Del Valencia CF mnamo Jumatano 25,2024.
Image: X// Harambee Starlets

Timu ya taifa ya wanadada wasiozidi umri wa miaka 17, Ijumaa watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Ureno kuanzia saa kumi na moja majira ya Afrika Mashariki.

Timu hiyo chini ya uongozi wa kocha Mildred Cheche ipo nchini Uhispania kwa mazoezi ya ziada wanapojiandaa kushiriki mashindano ya FIFA ya wanadada wasiozidi umri wa miaka 17.

Mechi hiyo itakuwa ya pili kwa Junior Starlets wakiwa nchini Uhispania baada ya kucheza mechi ya kwanza mnamo Jumatano dhidi ya Ciudad Deportiva Del Valencia.

Mechi hiyo, kikosi cha Kenya kilishinda kwa mabao manne kwa moja ambapo Valarie Nekesa alifunga mabao mawili katika dakika ya 9 na 26 huku Lindey Atieno akifunga mawili dakika za 35 na 56.

Junior Starlets imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya taifa ya Kenya kufuzu kombe la dunia katika historia ya soka ya Kenya.

Kocha Cheche ana siku chini ya 20 ya maandalizi ya FIFA itakayofanyika nchini Dominican Republic kuanzia Oktoba 16.

Junior Starlets inaendelea kukita kambi nchini Uhispania kwa ambapo watamaliza siku kumi moja za mazoezi kabla ya kyrejea nchini na hatimaye kuelekea Domican Republic.