Kiungo wa Manchester City na timu ya Uhispania Rodrigo Hernández Cascante ampiku Vinicius Jr wa Real Madrid na Jude Bellingham kushinda tuzo la mchezaji bora duniani Ballon d'Or. Rodri ambaye ameweka rekodi kwa taifa la Uhispaniakuwa mchezaji wa hivi punde kushinda tuzo hilo tangia mwaka wa 1960.
Rodri mwenye umri wa miaka 28 amekuwa kiungo muhimu kwa klabu yake ya Man City vile vile na timu yake ya taifa.Rodri ameisadia klabu ya Manchester City kushinda taji la ligu kuu Uingereza mfulilizo kwa mara nne.Aidha, aliisaidia timu ya taiga Uhispania kufika fainali la Euro 2024 na hatimaye kutwaa taji hilo.
Rodri baaada ya kushinda taji hilo alisema kuwa wachezaji wenza ndio ambao wamemsaidia pakubwa taji hili.
"Sitaki kuwasahau wachezaji wenza,Manchester City nawashukuru sana nyinyi ni watu spesheli ,najua singefaulu kama sio nyinyi.Kwangu mimi hii ndio klabu bora duniani kwa sasa,pia ningependa kushukuru timu ya taifa na pia kocha De la Fuente kwa kuniamini kwa mda mrefu,Kwa wenzangu ambao tulifanikiwa kushinda Euro, Carvajal na pia kinda Lamine ambaye nina imani utashinda taji hili hivikaribuni".
Aidha, mchezaji ambaye alionekana kushinda tuzo hilo Vinicius jr, hakuudhuria sherehe hizo baada ya kupata habari kuwa hakuwa mshindi wa tuzo hilo.Rodri Kushinda taji hilo amekuwa wa pili kama kiungo baada ya Luka Modric mwaka 2018.
Tangia mwaka 2023, Rodri amecheza jumla ya mechi 63 huku akifunga mabao 12 akitoa pasi zilizozalisha mabao 14. Aidha Rodri amepoteza michuano minne kwa klabu na taifa.