logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tazama orodha kamili ya matokeo ya tuzo ya Ballon d'Or

Vinicius Junior wa Real Madrid alipigiwa upato sana katika makadirio ya watu wengi

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Football29 October 2024 - 10:43

Muhtasari


  •  Kama kawaida, kulikuwa na makadirio na mjadala mkali kuhusu nani angeshinda tuzo za juu, huku kukiwa na utata mkubwa kuhusu tuzo ya wanaume.
  • Vinicius, wachezaji mwenzake na kambi nzima ya Real Madrid walikosa kuhudhuria hafla ya tuzo baada ya kujua matokeo mapema.

Tuzo za Ballon d'Or za mwaka wa 2024  zilipeanwa katika hafla kubwa ya kufana kwenye Ukumbi wa Theatre du Chatelet jijini Paris, Ufaransa mnamo Jumatatu, Oktoba 28.

 Kama kawaida, kulikuwa na makadirio na mjadala mkali kuhusu nani angeshinda tuzo za juu, huku kukiwa na utata mkubwa kuhusu tuzo ya wanaume ambayo Lionel Messi alishinda kwa mara ya nane mnamo 2023.

 Vinicius Junior alipigiwa upato sana katika makadirio ya watu wengi, kutokana na mwaka mzuri katika klabu yake ya Real Madrid - ambayo alishinda La Liga na Ligi ya Mabingwa na - na timu ya taifa ya Brazil.

 Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, kiungo wa Manchester City Rodri alinyakua tuzo hiyo huku Mbrazil huyo akiibuka wa pili na mwenzake Jude Bellingham akiibuka wa tatu.

 Vinicius, wachezaji mwenzake na kambi nzima ya Real Madrid walikosa kuhudhuria hafla ya tuzo baada ya kujua matokeo mapema.

 Hii hapa ni orodha kamili ya jinsi wateule walivyoorodheshwa katika utoaji tuzo:

  • 1 - Rodri (Spain, Manchester City)
  • 2 - Vinícius Júnior (Brazil, Real Madrid)
  • 3 - Jude Bellingham (England, Real Madrid)
  • 4 - Dani Carvajal (Spain, Real Madrid)
  • 5 - Erling Haaland (Norway, Manchester City)
  • 6 - Kylian Mbappé (France, Paris Saint-Germain / Real Madrid)
  • 7 - Lautaro Martínez (Argentina, Inter)
  • 8 - Lamine Yamal (Spain, Barcelona)
  • 9 - Toni Kroos (Germany, Real Madrid)
  • 10 - Harry Kane (England, Bayern Munich)
  • 11 - Phil Foden (England, Manchester City)
  • 12 - Florian Wirtz (Germany, Bayer Leverkusen)
  • 13 - Dani Olmo (Spain, Leipzig / Barcelona)
  • 14 - Ademola Lookman (Nigeria, Atalanta)
  • 15 - Nico Williams (Spain, Athletic Club)
  • 16 - Granit Xhaka (Switzerland, Bayer Leverkusen)
  • 17 - Federico Valverde (Uruguay, Real Madrid)
  • 18 - Emiliano Martínez (Argentina, Aston Villa)
  • 19 - Martin Odegaard (Norway, Arsenal)
  • 20 - Hakan Çalhanoğlu (Turkey, Inter)
  • 21 - Bukayo Saka (England, Arsenal)
  • 22 - Antonio Rüdiger (Germany, Real Madrid)
  • 23 - Ruben Dias (Portugal, Manchester City)
  • 24 - William Saliba (France, Arsenal)
  • 25 - Cole Palmer (England, Manchester City / Chelsea)
  • 26 - Declan Rice (England, Arsenal)
  • 27 - Vitinha (Portugal, Paris Saint-Germain)
  • 28 - Alejandro Grimaldo (Spain, Bayer Leverkusen)
  • 29= Mats Hummels (Germany, Borussia Dortmund)
  • 29= Artem Dovbyk (Ukraine, Dnipro / Girona / Roma)




RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved