Ikiwa wewe ni mfuasi wa soka, unapofikiria kuhusu mchezaji wa kulipwa; pengine unachoona ni ustadi, pesa, mtindo wa maisha wa kifahari, magari, mitindo na vitu vingine vya dhamani.
Kwa miaka mingi, wanasoka, haswa wale wanaocheza katika ligi kuu ulimwenguni wameonyesha maisha ya kifahari. Hii imesababishwa na mfuko mkubwa ambao wengi wao hupeleka nyumbani kila wiki, kila mwezi au kila mwaka.
Licha ya kucheza mchezo same, wanasoka hata hivyo wanapokea mishahara tofauti sana. Kulingana na Indeed.com, wataalamu katika uwanja huu wanalipwa kulingana na ujuzi, sifa, umaarufu, soko na mahitaji, nafasi wanayocheza, kandarasi na kanusho na rasilimali za kifedha za kilabu.
Forbes wanaripoti kwamba Saudi Pro League ndipo ambapo wanasoka wanavuna makubwa huku wanasoka wanne kati ya wanaocheza huko wakiorodheshwa miongoni mwa wachezaji kumi wanaolipwa zaidi. Ligi Kuu ya Uingereza ina wachezaji watatu katika orodha ya wachezaji kumi wanaolipwa pesa nyingi zaidi, La Liga ya Uhispania ina wawili huku nahodha wa Argentina Lionel Messi akiwakilisha Ligi Kuu ya Soka ya Marekani katika orodha hiyo.
Hivi leo, nyota wa Ureno Christiano Ronaldo anaendelea kuongoza orodha ya wanasoka wanaolipwa fedha nyingi kwa mara ya sita katika muongo uliopita huku mpinzani wake mkuu Lionel Messi akishika nafasi ya pili.
Mapato ya Ronaldo yanakadiriwa kuwa dola milioni 220 uwanjani msimu huu na zinaweza kufikia takriban dola milioni 285 ambazo anapata kutoka nje ya uwanja. Huu ni uboreshaji wa jumla ya $ 260 milioni alizokuwa akipata kwenye orodha ya Forbes 2023.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji 10 wa soka wanaolipwa zaidi mwaka 2024, kulingana na Forbes:
Cristiano Ronaldo: Umri: 39, Klabu: Al Nassr, Timu ya Taifa: Ureno
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno alihamia Saudi Pro League Januari 2023, huku Al-Nassr wakimpa kitita kikubwa cha pesa kuwachezea. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 anakadiriwa kutwaa dola milioni 220 kutokana na makusanyo ya uwanjani na ana mapato ya nje ya uwanja ya $65 milioni.
Lionel Messi: Umri: 37, Klabu: Inter Miami, Raia: Argentina
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona kwa sasa anachezea Inter Miami katika Ligi Kuu ya Soka ya Marekani (MLS), ambapo anafurahia mapato ya kila mwaka ya ndani ya uwanja ya dola milioni 60 na mapato ya nje ya uwanja $75 milioni.
Neymar Jr: Umri: 32, Klabu: Al Hilal, Raia: Brazil
Nyota
huyo wa Brazil aliwaaga wababe wa Ufaransa Paris Saint-Germain na kujiunga na
Al Hilal mnamo Agosti 2023. Akiorodheshwa
kama mchezaji wa tatu wa kipato cha juu mwaka huu, ana mapato ya ndani ya dola 80
milioni na mapato ya nje ya uwanja ya $ 30 milioni.
Karim Benzema: Umri: 36, Klabu: Al Ittihad, Raia: Ufaransa
Nyota wa Ufaransa Karim Benzema ameorodheshwa katika nafasi ya nne akiwa na mapato ya ndani ya $100 milioni na nje ya uwanja ya $4 milioni.
Kylian Mbappe: Umri: 25, Klabu: Real Madrid, Raia: Ufaransa
Mbappe alitimiza ndoto yake alipojiunga na klabu yake ya utotoni ya Real Madrid mapema mwaka huu. Sio tu kwamba ndoto yake ilitimia, lakini mapato yake yalipanda hadi $ 70 milioni katika mkusanyiko wa uwanjani na $ 20 milioni nje ya uwanja.
Erling Haaland: Umri: 24, Klabu: Manchester City, Raia: Norway
Mshambulizi bora wa Man City Erling Haaland ameorodheshwa kama mchezaji wa sita wa kandanda anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani na wa kwanza kwenye EPL akiwa na mapato ya ndani ya uwanja ya $46 milioni na mapato ya nje ya uwanja $14 milioni.
Vinicius
Jr: Umri: 24, Klabu: Real Madrid, Raia: Brazil
Nyota huyo wa Real Madrid anakuwa Mbrazil wa pili katika orodha ya wanasoka wanaolipwa fedha nyingi zaidi akiwa na mapato ya ndani ya $40 milioni na $15 milioni nje ya uwanja.
Mohamed
Salah: Umri: 32, Klabu: Liverpool, Raia: Misri
Mo Salah sio tu mchezaji wa nane wa soka anayelipwa zaidi duniani, lakini ndiye mchezaji wa juu zaidi barani Afrika. Ana mapato ya ndani ya $35 milioni na mapato ya nje ya uwanja $18 milioni.
Sadio
Mane: Umri: 32, Klabu: Al Nassr, Raia: Senegal
Nyota huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 32 ni Mwafrika wa pili kwenye orodha hiyo akiwa na mapato ya ndani ya $48 milioni na mapato ya nje ya uwanja $4 milioni.
Kevin De Bryune: Umri: 33, Klabu: Manchester City, Raia: Ubelgiji
Anayefunga orodha ya wachezaji kumi wanaopata pesa nyingi zaidi katika ulimwengu wa kandanda ni nahodha wa Manchester City, ambaye anakadiriwa mapato ya kila mwaka ya ndani ya $35 milioni na $4 milioni nje ya uwanja.