Denis Omedi, mcezaji wa kabumbu wa timu ya Kitara na timu ya taifa ya Uganda, ameteuliwa kuwania tuzo ya Puskas ya mwaka huu kutokana na bao alilofunga katika mechi kati ya timu yake Kitara dhidi ya KCCA mwezi Agosti tarehe 6 kwenye mashindano ya Ugandan Super 8.
Omedi yupo katika orodha ya wachezaji 11 ambao walifunga mabao ya kuustaajabisha au yasiyo ya kawaida kwenye ulimwengu wa soka.
Bao alilofunga Dennis Omedi linatambulika kama ‘rabona’ ambapo mchezaji hupiga mpira kwa mguu ukiwa nyuma ya mguu mwingine. Bao kama hilo limewai kushinda tuzo ya Puskas ya mwaka 2021 ambapo mchezaji Erick Lamela aliifunga timu ya Arsenal kwenye debi wakati akichezea Tottenham Hotspurs.
Bao hilo la Omena liliisaidia timu ya Kitara kumaliza mechi
yao kwa sare ya kufungana mabao matatu.
Hata hivyo, Denis Omena anatarajia ushindani
mkubwa kutoka kwa wachezaji wengine waliocheza mechi mbali mbali duniani
ikiwemo Alejandro Garnancho wa Man United, Mohammed Kudus wa Westham na Jaden
Philogene wa Aston Villa.