Kaka wa Marcus Rashford akamatwa Marekani

Dane Rashford alikamatwa kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa nyumbani nchini Marekani.

Muhtasari

•Dane Rashford atafikishwa mahakamani hivi karibuni kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa nyumbani nchini Marekani.

• Marcus Rashford alitolewa nje wakati wa mechi ya Manchester United dhidi ya Copenhagen FC Jumatano usiku.

katika picha ya maktaba.
Marcus Rashford na kaka yake Dane Rashford katika picha ya maktaba.
Image: HISANI

Dane Rashford, kaka mkubwa wa mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford atafikishwa mahakamani hivi karibuni kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa nyumbani nchini Marekani.

Taarifa kutoka Uingereza zinasema kuwa Dane, ambaye pia ni meneja wa mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 26, alikamatwa mnamo Oktoba 20 katika Miami Beach, Florida na alifikishwa mahakamani siku iliyofuata.

Msimamizi huyo wa Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 31 aliachiliwa kwa bondi ya dola 1,224 (Ksh 185,436) kabla ya kusikilizwa kwa kesi yake, kulingana na rekodi za polisi.  Dhamana ya kuachiliwa kwake ililipwa na Chantelle Maynard wiki moja baada ya kukamatwa, na sasa Dane Rashford hayuko tena gerezani na amekana mashtaka. Ana kesi nyingine mwishoni mwa mwezi huu, mnamo Novemba 27.

Kulingana na Telegraph, shtaka lake baadaye lilisajiliwa Oktoba 24 kama utovu wa nidhamu, ambao ulifafanuliwa zaidi kama unyanyasaji wa nyumbani.

Mkurugenzi huyo wa Usimamizi wa Michezo wa DN May ambaye anawakilisha Marcus Rashford, ambaye picha yake ya mashtaka ilichukuliwa, amepewa agizo la kabla ya kesi "kukaa mbali" na Jimbo la Florida, ambalo linadaiwa kutoruhusu mawasiliano yoyote.

Gazeti la Telegraph linaripoti kwamba familia ya Rashford inasema suala hilo limetatuliwa lakini mwendesha mashtaka msaidizi wa jimbo la Miami Dade, Daysi Vega-Mendez, anasema kesi bado iko. Vega-Mendez anasema tukio hilo liliaminika kutokea wakati Dane Rashford alipokuwa likizoni katika Jimbo la Sunshine.

Wakati ripoti za kukamatwa kwa Dane zikiibuka, kaka yake mdogo Marcus Rashford alitolewa nje wakati wa mechi ya Manchester United dhidi ya Copenhagen FC Jumatano usiku.

Rashford alicheza kwa dakika 40 pekee kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi Donatas Rumsas kufuatia kumchezea vibaya mchezaji wa Copenhagen Elias Jelert,

Manchester United iliendelea kupoteza mechi hiyo 4-3 na kuwapeleka hadi chini ya kundi A.