logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kunani? Bahati apost picha ya Diana Marua na mwanasoka mashuhuri, na ku’unfollow Diana

Je, kunaweza kuwa na shida katika ndoa hiyo ya zaidi ya miaka saba au wanatafuta kiki tu?

image
na Radio Jambo

Football04 June 2024 - 04:01

Muhtasari


•Chapisho hilo limeibua hisia mseto kutoka kwa mamia ya watumiaji wa mitandao ambao wengi wameonekana kutaka kujua madhumuni ya hatua hiyo.

•Bahati aliacha kumfuatilia Diana Marua kwenye mtandao wa Instagram, hatua ambayo imezua wasiwasi zaidi kuhusu ndoa yao.

Mwimbaji Kelvin Kioko almaarufu Bahati amezua utata baada ya kuchapisha picha ya maktaba ya mkewe Diana Marua akibarizi na mchezaji mashuhuri wa zamani wa Harambee Stars.

Msanii huyo wa zamani wa nyimbo za injili alishiriki picha hiyo isiyojulikana wazi ilipigwa lini kwenye kurasa zake zote za mitandao ya kijamii  siku ya Jumatatu jioni na kuiambatanisha na ujumbe wa kutia wasiwasi.

Chini ya picha hiyo, alichapisha emojis za moyo uliovunjika, ambazo mara nyingi hutumiwa kuashiria huzuni.

“💔💔💔💔💔💔,” Bahati aliandika kwenye picha hiyo.

Chapisho hilo limeibua hisia mseto kutoka kwa mamia ya watumiaji wa mitandao ambao wengi wameonekana kutaka kujua madhumuni ya hatua hiyo.

Tazama maoni kutoka kwa baadhi ya watumiaji  wa Instagram;

Terencecreative: Alaaa???

Milly_wairimu: Ikiwa huu ni utani basi ni ghali sana Baha.

Daphney_amisi: Toa Ngoma mzee, tuko tayari.

Janet_william0: Kufuatilia kwa karibu.

Hypejosh_: Bro unapaswa kuwalinda wapendwa wako @bahatikenya

Pamoja na kupost chapisho hilo la kutiliwa shaka, mwimbaji huyo wa nyimbo za mapenzi pia alichukua hatua ya kuacha kumfuatilia Diana Marua kwenye mtandao wa Instagram, hatua ambayo imezua wasiwasi zaidi kuhusu ndoa yao.

Ukaguzi wa haraka katika akaunti ya Instagram ya Diana Marua pia unathibitisha kwamba yeye pia hamfuatilii tena mumewe kwenye jukwaa hilo la mtandao wa kijamii.

Je, kunaweza kuwa na shida katika ndoa hiyo ya zaidi ya miaka saba au wanatafuta kiki tu? Naam, itabidi tusubiri ili kujua.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved