Tazama kikosi cha Chelsea cha wachezaji 41; makipa 6, mabeki 11, viungo 10 na washambuliaji 14

Klabu hiyo sasa ina kikosi cha wachezaji wasiopungua 41.

Muhtasari

•Chelsea walifanya usajili wao wa hivi punde zaidi kwa kumleta kipa Mike Penders kutoka Genk kwa ada inayoaminika kuwa karibu £17m.

•EPL imewatambua wachezaji 41 ndani ya Chelsea kwa sasa wanaojumuisha makipa 6, mabeki 11, viungo 10 na washambuliaji 14.

Image: HISANI

Siku ya Jumanne, Agosti 27, Chelsea walifanya usajili wao wa hivi punde zaidi kwa kumleta kipa Mike Penders kutoka Genk kwa ada inayoaminika kuwa karibu £17m.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 atajiunga rasmi kwa mkataba wa muda mrefu hadi 2032 katika majira ya joto ya 2025, na kuwa kipa wa tisa katika klabu hiyo yenye makao yake London.

Atakuwa mchezaji mpya zaidi katika kikosi kikubwa cha washindi hao wa Ligi ya Mabingwa 2020/21.

Klabu hiyo sasa ina kikosi cha wachezaji wasiopungua 41.

Ligi Kuu ya Uingereza, kupitia tovuti yao rasmi, imewatambua wachezaji 41 ndani ya Chelsea kwa sasa wanaojumuisha makipa 6, mabeki 11, viungo 10 na washambuliaji 14.

Tazama orodha nzima ya wachezaji 41 wa Chelsea katika tovuti rasmi ya Ligi Kuu ya Uingereza;

  1. Kepa (Kipa) Hispania
  2. Marcus Bettinelli (kipa) England
  3. Robert Sanchez (Kipa) Uhispania
  4. Lucas Bergström (kipa) Finland
  5. Djordje Petrovic (kipa)Serbia
  6. Filip Jørgensen (kipa) Denmark
  7. Axel Disasi (Beki) Ufaransa
  8. Marc Cucurella (Beki) Uhispania
  9. Benoît Badiashile (Beki) Ufaransa
  10. Trevoh Chalobah (Beki) Uingereza
  11. Ben Chilwell (Beki) Uingereza
  12. Reece James (Beki) Uingereza
  13. Levi Colwill (Beki) Uingereza
  14. Josh Acheampong (Beki) Uingereza
  15. Malo Gusto (Beki) Ufaransa
  16. Wesley Fofana (Beki) Ufaransa
  17. Tosin Adarabioyo (Beki) Uingereza
  18. Enzo Fernandez (Kiungo wa kati) Argentina
  19. Mykhailo Mudryk (Kiungo wa kati) Ukraine
  20. Carney Chukwuemeka (Kiungo wa kati) Uingereza
  21. Kiernan Dewsbury-Hall (Kiungo wa kati) Uingereza
  22. Renato Veiga (Kiungo wa kati) Ureno
  23. Cole Palmer (Kiungo wa kati) Uingereza
  24. Moisés Caicedo (Kiungo wa kati) Ecuador
  25. Cesare Casadei (Kiungo wa kati) Italia
  26. Roméo Lavia (Kiungo wa kati) Ubelgiji
  27. Tino Anjorin (Kiungo) Uingereza
  28. Romelu Lukaku (Mshambuliaji) Ubelgiji
  29. Raheem Sterling (Mshambuliaji) Uingereza
  30. Noni Madueke (Mshambuliaji) Uingereza
  31. Nicolas Jackson (Mshambuliaji) Senegal
  32. Christopher Nkunku (Mshambuliaji) Ufaransa
  33. Armando Broja (Mshambuliaji) Albania
  34. Deivid Washington (Mshambuliaji) Brazil
  35. Tyrique George (Mshambuliaji) Uingereza
  36. Omari Kellyman (Mshambuliaji) Uingereza
  37. David Datro Fofana (Mshambuliaji) Cote D’Ivoire
  38. Ângelo (Mshambuliaji) Brazil
  39. Marc Guiu (Mshambuliaji) Uhispania
  40. Pedro Neto (Mshambuliaji) Ureno
  41. João Félix (Mshambuliaji) Ureno