•Baada ya msimu wa kukumbukwa wa 2023-24, orodha fupi ya walioteuliwa kuwania tuzo hilo la kifahari mwaka wa 2024 imetangazwa.
•Ni vizuri kuona majina mapya katika orodha hiyo baada ya miongo 2 ya utawala wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao wote sasa wako nje ya orodha.
Orodha ya walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji binafsi ya kifahari zaidi duniani, Ballon d’Or, imefichuliwa kabla ya hafla ya tuzo kufanyika mjini Paris, Ufaransa mnamo Oktoba 28, 2024.
Ballon d'Or bila shaka ndiyo tuzo ambayo kila mwanasoka duniani ana ndoto ya kushinda siku moja. Baada ya msimu wa kukumbukwa wa 2023-24, orodha fupi ya walioteuliwa kuwania tuzo hilo la kifahari mwaka wa 2024 imetangazwa.
Kuna baadhi ya wanasoka mahiri wanaowania kutwaa tuzo hiyo ambayo Lionel Messi alitwaa kwa mara ya nane mwaka 2023, huku matokeo si tu katika ngazi ya vilabu, bali pia katika michuano mbalimbali mikubwa iliyofanyika katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, yakizingatia wakati wa kuchagua orodha ya mwaka huu ya washindi wanaotarajiwa.
Wachezaji wawili wa Real Madrid, Jude Bellingham na Vinicius Junior wamependekezwa sana kushinda tuzo hilo, huku wawili hao wakiwa na mafanikio mengi msimu uliopita.
Erling Haaland, Phil Foden, Nico Williams na Lamine Yamal wote pia watakuwa miongoni mwa wale wanaotarajia kumaliza katika nafasi bora kwenye tuzo hizo.
Ni vizuri kuona baadhi ya majina mapya katika orodha hiyo baada ya miongo miwili ya utawala wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao wote sasa wako nje ya orodha.
Tazama orodha kamili ya wanasoka wa kiume walioteuliwa kuwania tuzo hiyo ya kifahari:-
- Jude Bellingham - Real Madrid/England
- Ruben Dias - Man City/Portugal
- Phil Foden - Man City/England
- Federico Valverde - Real Madrid/Uruguay
- Emiliano Martinez - Aston Villa/Argentina
- Erling Haaland - Man City/Norway
- Nico Williams - Athletic Club/Spain
- Granit Xhaka - Bayer Leverkusen/Switzerland
- Artem Dovbyk - Girona/Roma/Ukraine
- Toni Kroos - Real Madrid/Germany
- Vinicius Junior - Real Madrid/Brazil
- Dani Olmo - RB Leipzig/Barcelona/Spain
- Florian Wirtz - Bayer Leverkusen/Germany
- Martin Odegaard - Arsenal/Norway
- Mats Hummels - Borussia Dortmund/Roma/Germany
- Rodri - Man City/Spain
- Harry Kane - Bayern Munich/England
- Declan Rice- Arsenal/England
- Vitinha - PSG/Portugal
- Cole Palmer - Chelsea/England
- Dani Carvajal - Real Madrid/Spain
- Lamine Yamal - Barcelona/Spain
- Bukayo Saka - Arsenal/England
- Hakan Calhanoglu - Inter/Turkey
- William Saliba - Arsenal/France
- Kylian Mbappe - PSG/Real Madrid/France
- Lautaro Martinez - Inter/Argentina
- Ademola Lookman - Atalanta/Nigeria
- Antonio Rudiger - Real Madrid/Germany
- Alejandro Grimaldo - Bayer Leverkusen/Spain