Shujaa 7s wang'aa kwenye michuano ya Vancouver 7s

Muhtasari

•Shujaa walinyakua pointi 18 baada ya kulemewa nguvu na wenzao wa Afrika Kusini katika fainali ya mashindano hayo. 

•Hapo awali timu hiyo ambayo inaongozwa na kocha Innocent Simiyu ilikuwa imepata ushindi wa 17-5 dhidi ya Uhispania, 45-7 dhidi ya Mexico na 19-14 dhidi ya Marekani kwenye robo fainali.

Image: WORLD RUGBY SERIES

Timu ya taifa ya raga almaarufu kama Shujaa 7s wameibuka katika nafasi ya pili kwenye michuano ya Seven's World Series 2021/22 ambayo ilikuwa inafanyika jijini Vancouver, Canada kati ya Ijumaa na Jumatatu.

Shujaa walinyakua pointi 18 baada ya kulemewa nguvu na wenzao wa Afrika Kusini katika fainali ya mashindano hayo. The Springboks walishinda shujaa kwa pointi 38-5 kwenye mchuano ambao ulichezwa mida ya saa tisa unusu usiku wa kuamkia Jumatatu.

Shujaa walikuwa wameshinda Ireland kwa pointi 38-5 katika nusu fainali na kuhitimu kuingia fainali ya michuano ya kwanza ya msimu mpya wa raga.

Hapo awali timu hiyo ambayo inaongozwa na kocha Innocent Simiyu ilikuwa imepata ushindi wa 17-5 dhidi ya Uhispania, 45-7 dhidi ya Mexico na 19-14 dhidi ya Marekani kwenye robo fainali.

Springboks wa Afrika Kusini walimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye michuano ya Vancouver 7s na pointi 20.

Michuano ya World Series itaendelea jijini Edmonton, Canada wikendi ijaayo.