Miguna Is Back!: Serikali yaagizwa kufanikisha kurejea kwa Wakili Miguna Miguna

  • Wizara ya usalama wa ndani imesema itatii agizo la mahakama kumruhuhusu Miguna  kuingia nchini .

  • Msemaji wa serikali Cyrus Oguna a Jumapili alisema serikali haitoingia kuwasili nchini kwa wakili huyo .

Mahakama kuu Jumatatu imetoa agizo kwa serikali kufanikisha kurejea nchini kwa wakili Miguna Miguna siku ya jumanne .  Jaji Weldon Korir  ameziagiza idara za DCI ,uhamiaji na Polisi kutoingilia kwa vyovyote juhudi za Miguna kurejea humu nchini .Korir  pia amemwagiza msajili wa mahakama kuikabidhi paspoti ya Miguna kwa wakili wake au afisa yeyote wa tume ya kitaifa ya haki za binadamu .

Wakati huo huo kupitia kwa taarifa iliyotumwa kwa vuombo vya habari  ,wizara ya usalama wa ndani ilisema inalenga kutii agizo la mahakama kwa kumruhusu Miguna arejee nchini bila bughdha . Awali siku ya jumapili msemaji wa serikali Cyrus Oguna alisema serikali haina nia ya kuingilia   mpango wa Miguna kuja Kenya .Hatua hiyo sasa inatuliza hofu ya kuzuka patashika nyingine kama ilivyoshuhudiwa  hapo awali wakati Miguna alipotangaza nia yake ya kutaka kurejea Kenya . Wakili huyo mtatanishi  alifurushwa nchini na vyombo vya usalama mnamo Februari mwaka wa 2018 .

Hatua hiyo ya serikali kulegeza msimamo kuhusu kuja nchini wa Miguna imetokea baada ya wakili huyo mwenye yake  jijini Torono kutangaza kwamba atawasili katika uwanja wa ndege ya JKIA ,Nairobi saa tatu isiku siku ya Jumanne .  Pindi alipotangaza mpango wake wa kutaka kurejea nchini ,Miguna alijipata mtandaoni akilalamika kwamba polisi walikuwa  wamelinasa gari lake  katika hatua za kumtishia asifike Kenya . Miguna alihamishwa hadi Cabada  baada ya kuzuiliwa na polisi kwa siku tano kuhusu wajibu wake katika kumuapisha kiongozi wa ODM  Raila Odinga  kama ‘ Rais wa watu’ Januari  ,30 2018 .