Miguna Miguna huenda akajipata katika malumbano na serikali atakaporejea Jumanne

Wakili Miguna Miguna huenda tena akajipata katika malumbano na serikali atakaporejea nchini siku ya jumanne baada ya kudai mtandaoni kwamba polisi wamelinasa gari lake hapo jana jumamosi.

Miguna amesema maafisa wa polisi waliokuwa na nguo za raia walilitwaa gari hilo mtaani South B katika hatua anayodai inalenga kuhujumu kurejea kwake nchini. Aliripoti baadaye kwamba polisi waliamua kuliachilia gari hilo.

Mkusanyiko wa habari,

Makachero wamensa runinga 37 zinazoshukiwa kuwa shemu ya vifaa vya elektroniki vyenye thamani ya shilingi milioni 5 vilivyoibwa huko Athi River tarehe moja disemba mwaka jana mshukiwa mmoja kwa jina John Maina amekamatwa na atafikishwa kortini hapo kesho.

Iwapo umekuwa na mfanyikazi wa nyumbani kwa zaidi ya miezi mitatu basi unahitaji kusaini mkataba naye. Wakili Anne Babu  anasema sheria inamhitaji mtu kumpa mkataba mfanyikazi wake wa nyumbani baada ya miezi mitatu.

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi amesema wakenya wengi wanahangaika kwa sababu ya haLi mbaya ya uchumi na sera mbovu za serikali ya Jubilee. Sudi amedai kwamba wazazi wengi hawana fedha za kuwalipia wanao karo shuleni ilhali shule zinafunguliwa kesho.

Amedai kwamba utawala wa rais Uhuru Kenyatta umewafanya wakenya kupitia hali mbaya zaidi kiuchumi katika historia ya taifa.

Waziri wa elimu George Magoha ametishia kukifunga kiwanda cha sukari cha kibos endapo usimamizi wake utakosa kuihamisha shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalum hadi katika sehemu nyingine katika mji wa Kisumu. Magoha amesema wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule hiyo wanaendelea kuhaingaika kwa ajili ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na kiwanda hicho umbali wa mita 20 kutoka shule hiyo.

MkurUgenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji amemtuma mwendesha mashtaka mwingine katika mahakama ya kilungu baada ya kisa cha ijumaa Ambapo afisa mmoja wa mahakama alijitosa kortini na kuchukua faili za kesi na kisha kuondoka nazo. mwendesha mashtaka huyo anayedaiwa kuwa mlevi alilemaza shughuli za korti na kumwacha kinywa wazi hakimu mkaazi Elizabeth Muiru.

Wafanyibiashara kadhaa huko machakos wanakadiria hasara waliopata jana baada ya moto kuteketeza jengo lenye biashara zao. Afisa wa kusimamia majanga David Mwongela amesema juhudi za zima mto kukabiliana na moto huo zilipata pigo baada ya maafisa wa Kenya power kuchelewa kufika ili kuzima umeme.