EXPtHi7XYAADEcr

Miili ya maafisa 7 waliosombwa na mafuriko yapatikana

NA NICKSON TOSI

Mkiili ya maafisa 7 wa polisi waliosombwa na mafuriko  pamoja na lori walilokuwa wanatumia eneo la Chemeo kaunti ya Baringo hatimaye imepatikana.

Shughuli ya kutafuta miili ya maafisa hao sasa ilikuwa imedumu kwa wiki moja, baada ya mratibu wa serikali George Natembeya kusema kuwa mvua kubwa inayoshudiwa maeneo ya Rift Valley ilikuwa inawatoa kijasho cha kutafuta miili hiyo.

Maafisa 7 wa polisi hawajulikani waliko baada ya gari lao kusombwa na mafuriko

Image

Maafisa hao saba walisombwa ma mafuriko hayo walipokuwa wanaenda kushika doria eneo hilo la Chemoe kabla ya ya kukutana na kifo chao.

Maelfu ya watu nchini wameathirika pakubwa na mvua inayoendelea kunyesha kote huku wengine wakipoteza maisha yao kutokana na mvua hiyo.

Kivuko cha Mauti! Watu wanne waangamia baada ya boti kupinduka mto Kerio

Kaunti za Rift Valley, Magharibi na Nyanza ndizo zilizoathirika pakubwa kufikia sasa.

Aidha katika kaunti ya Elgiyo Marakwet serikali ililazimika kutumia DNA ili kubaini baadhi ya miili baada ya sehemu za miili ya wale walioafariki kuwa vibande .

 

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments