OUT AT LAST!Miili ya Mama na Bintiye hatimaye yaondolewa Bahari Hindi

  Gari  lililoanguka  katika bahari Hindi likiwa na  na mama na binti yake limeondolewa  majini .Miili ya Miriam  Kighenda na binti yake Amanda Mutheu  ilipatikana katika kiti cha nyuma cha gari hilo . Wawili hao waliaga dunia pamoja wakiwa wamekumbatiana  .Wachunguzi wamekuwa  na wakati  mgumu kuitenganisha miili ya wawili hao .  Gari lao liliteleza kutoka kwenye feri ya MV Harambee tarehe 30 mwezi septemba  katika kivuko cha Likoni  na kutumbukia baharini .

Tangia wakati huo serikali na idara mbali mbali za usalama wa majini wakiwemo wapiga mbizi wa kibinafsi wamekuwa wakiendelea na juhudi za kuiondoa miili hiyo pamoja na gari hilo bila mafanikio .Siku ya jumatano msemaji wa serikali Cyrus Oguna kwa mara ya kwanza alitoa matumaini kwa familia na wakenya kwa kutangaza kwamba kifaa kinachofanana na gari kilionekana umbali wa mita zaidi ya 50 chini ya bahari na kutoa fursa ya oparesheni ya leo kuliondoa gari hilo .

John Wambua ,mume wa marehemu Miriam Kighenda na ambaye pia alimppteza binti yake Amanda Mutheu katika mkasa wa Likoni

Gari hilo lilivutwa kwa kreni katika oparesheni iliyochukua saa nane na kufikia saa kumi na dakika 12 ijumaa ,gari lenyewe liliondolewa na kuwekwa ardhini . Mumewe Miriam ,John Wambua alikuwa katika eneo la mkasa wakati  gari gilo lilipokuwa likivutwa kutoka baharini .Umati wa watu ulijaa katika fuo za bahari kujionea oparesheni hiyo licha ya polisi kuwaondoa mamia ya wananchi waliokuwa na hamu ya kushuhudia shughuli ya kuondoa gari hilo .