Miili ya walioga dunia kwa ajili ya Covid-19 yafukuliwa na kuzikwa upya na wazee wa jamii ya bukusu

kifo
kifo
Miili ya watu waliofariki kwa ajili ya covid 19  magharibi mwa Kenya inafukuliwa na jamaa zao na kuzikwa upya kwa mujibu wa  mila za majii ya wabukusu .

Chini ya mwongozo wa wizara y afya kuhusu mazishi ya walioaga dunia kwa ajili ya ugonjwa huo  hafla za mazishi zilibadilishwa kuwa za saa moja tu huku watalaam waliovyalia magwanda ya kujikinga ndio wakiiweka mili ya wafu  katika kaburi .

Lakini kwa kuhofia laana , wazee wa jamii ya wabukusu wameamua kwenda kuifukua baadhi ya miili ya wapendwa wao na kuziika kwa ‘njia inayofaa’ kufuata utamaduni wa jamii yao .

Kulingana na desturi za jamii hiyo  kicha cha mfu kinafaa  kuangalia upande wa mabli na boma  vitu kama  viatu ,shati , au tai vinavyaa kulegezwa katika mwili wa marehemu .

Iwapo hilo halitafanywa inaamnika  mtu aliyefariki anawezxa kuitesafamilia yake  katika ndoto zao ,kulingana na wazee

Maazishi ya mtu mmoja mashuhuri yaliofanyika wiki  hii  yalihusisha familia ya mwanasiasa mmoja anayejulikana ambaye babake yupo katika baraza la wazee na walilazimika kuufukua mwili wa mpendwa wao na kisha kuuzikwa upya kwa mujibu wa desturi za jamii yao .

Mwenyekiti wa baraza hilo Patrick Chaka amesema jamii yake imejitolea kufuata mila hizo . Amesema jamii yao huwazika watu kutegema kilichosababisha vifo vyao .

Mtu anayeaga dunia kwa kujiua  au kwa kunywa sumu lazima acharazwe viboko kabla ya kuzikwa wakati wa usiku . wale wanaofariki kwa njia ya kawaida  huzikwa baada ya siku tatu na sio kabla ya saa tisa mchana kwa watu wazima .