Miili ya watoto 2 yapatikana Mto Nairobi

Nrb River
Nrb River
Miili ya watoto wawili imepatikana katika mto Nairobi.  Hatua hiyo imemfanya gavana wa Nairobi Mike Sonko kuwataka polisi kuwa waangalifu ili kuweza kuwatambua na kuwakamata watu ambao huitupa miili ya watu katika mto huo.

Miili ya watoto hao ilipatikana katika eneo la korogocho na kundi la vijana wanaousafisha mto Nairobi. Hatua hiyo sasa inafikisha 21 idadi ya jumla ya miili ya watu waliopatikana katika mto Nairobi.

Miili hiyo ni pamoja na ya watoto 16 na watu 5 wazima. Gavana Sonko amewataka wakaazi wanaoishi karibu na mto huo kuwa waangalifu ili kuweza kuwaripoti wanaoendeleza wovu huo.