Mike sonko afunguka kuhusu kesi zinazomwandama, asema haogopi

6roHCf0I_400x400
6roHCf0I_400x400
Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko sasa anasema kuwa haogopi na wala hatishwi na lolote katika vita dhidi ya ufisadi.

Mike ametangaza kuwa hajawahi kujificha kutoka kwa maafisa wa upelelezi.

Gavana huyu mwenye utata amewaomba wakaazi na viongozi kutosikitika kuhusu hali yake.

Soma hadithi nyingine;

Aidha amewataka viongozi wazidi kuchapa kazi na kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi na kuboresha jiji.

“Shida yangu ni shida yangu kama Sonko, si shida ya wakazi wala maendeleo ya Nairobi, kwa hivyo shida yangu mniachie,” alisema Sonko.

Sonko amesema kuwa yupo katika mstari kwa kwanza kumuunga mkono Rais Kenyatta na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji katika juhudi za kuangamizwa zimwi la ufisadi.

Aidha, kiongozi huyu amesema kuwa hatazungumzia lolote kuhusu tuhuma zinazomwandama hadi uchunguzi ukamilike,

Soma hadithi nyingine;

“Hii ni hali yangu, nyinyi muendelee na muungane mikono kama wakazi wa Nairobi, mimi sitaongea kitu kwa sasa hadi uchunguzi ukamilike,” alisema Bw Sonko.