Mike Sonko awashauri wanaume kuwapenda wake zao zaidi ya mipango ya kando.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amewashauri wanaume kujifunza jinsi ya kusawazisha upendo wanaowaonyesha mipango ya kando na ule wanaowapa wake zao. Sonko ambaye amekuwa kwenye ndoa kwa miaka 21 anasema siri ya kudumisha ndoa ni upendo na kuheshimiana.

Katika mtandao wa Instagram, Sonko anadai kuwa wanaume wanapswa kuwacha kuwapenda mipango ya kando zaidi ya wanavyowapenda wake zao. Anasema kwake yeye mke anafaa kupewa kipa umbele na kisha kila kitu kitakuwa sawa.

https://www.instagram.com/p/B0bZwJHhd2e/

Kwa mujibu wa Sonko ndoa inahitaji kusameheana na kuvumiliana. Hata hivyo baadhi ya wafuasi wake walihisi kwamba matamshi ya gavana huyo hayakuwa ya sawa kwani yanachangia uzinifu. Wengine walihisi kwamba alisema ukweli mtupu.

Sonko anajulikana kama kiongozi ambaye haoni haya kuweka bayana siri za kudumisha ndoa. Ameshawahi kuwashauri wanaume kuwa na tabia ya kuomba msamaha wanapowakosea wake zao. Pia aliwataka kuwa wanyenyekevu na wavumilivu iwapo wanataka kuwa na furaha.