ARTETA 1

Mikel Arteta: Mkufunzi wa Arsenal akutwa na ugonjwa wa coronavirus

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekutwa na virusi vya ugonjwa wa corona na mechi kati ya timu yake na Brighton iliyotarajiwa kuchezwa wikendi imeahirishwa.

 
The Gunners wamefunga uwanja wao wa mazoezi na wafanyakazi wa klabu hiyo ambao waligusana na Arteta wamelazimika kujiweka karantini.

 

Yafahamu Mataifa yote yaliyothibitisha visa vya Coronavirus

 

Ligi ya Premia itafanya mkutano wa dharura na klabu zote siku ya Ijumaa ili kuzungumzia kuhusu mechi zinazotarajiwa kuchezwa.

 
”Hii kwa kweli inasikitisha” , alisema raia wa Uhispania Arteta mwenye umri wa miaka 37.
”Niliamua kupimwa baada ya kujihisi vibaya lakini nitarudi kazini mara tu nitakaporuhusiwa kufanya hivyo”.

ODOI 1

 

Arsenal inatarajia kwamba idadi kubwa ya wafanyakazi na kikosi chote cha kwanza kitalazimika kujiweka karantini.

 

 

Klabu hiyo ilikuwa ikitarajiwa kukabiliana na Brighton katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza siku ya Jumamosi mwendo wa saa 11 jioni lakini Brighton ikatoa taarifa muda mfupi baada ya Arteta kugunduliwa ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo, ikitangaza kwamba mechi hiyo imeahirishwa.

OLIMP

BBC Sport inaelewa kwamba vilabu vyote vya ligi ya England vinataka kuamua kuhusu uamuzi wa pamoja na mojawapo ya uamuzi huo ambao utajadiliwa katika mkutano ni kuahirisha mechi zote zitakazochezwa wikendi hii.

 

VP wa Iran aambukizwa virusi vya Corona

 

”Afya ya watu wetu na umma kwa jumla ni jukumu letu na hapo ndipo tunapoangazia kwa sasa”, alisema mkurugenzi mkuu wa Arsenal Vinai Venkatesham.

 
”Tunaendelea na mazungumzo kwa wote wanaoshukiwa kupata maambukizi ili kukabiliana na hali vizuri, na tunatarajia kurudi katika mazoezi hivi karibuni pindi tu ushauri wa kiafya utakapoturuhusu”.

 
Mechi ya ligi ya Uingereza kati ya Arsenal na Manchster City pia imeahirishwa siku ya Jumatano kama hatua ya tahadhari kabla ya wachezaji kadhaa wa Arsenal kujiweka katika karantini baada ya mmiliki wa Olympiakos Evangelos Marinakis kuambukizwa virusi hivyo.

 
Arsenal ilisema kwamba Marinakis , 52 alikutana na wachezaji wake kadhaa wakati Arsenal ilipocheza mechi ya kombe la Yuropa dhidi ya Olympiakos katika uwanja wa Emirates wiki mbili zilizopita. Klabu hiyo ilisema kwamba hakuna mfanyakazi ama mchezaji atakayefanyiwa vipimo vya virusi vya corona.

 
Wakati huohuo, beki wa Manchester City Benjamin Mendy amejiweka katika karantini kama hatua za tahadhari baada ya nduguye mmoja kulazwa hospitalini akionesha dalili za ugonjwa wa corona.Wachezaji watatu wa Leicester City pia wamelazimika kujiweka katika karantini baada ya kuonesha dalili za ugonjwa huo.

 

MATCH

 

Ligi ya Uingereza inakaribia kuahirishwa. Kwa siku kadhaa sasa maafisa wakuu wameamini kwamba mechi zitachezwa bila ya mashabiki uwanjani huku maandalizi ya kufanya hivyo yakiwekwa mezani.

Kenya ina maabara mawili ya kupima virusi vya Corona

Licha ya kuwepo ukosoaji wa kuendelea na mechi bila ya kujali ugonjwa huo tofauti ya inavyofanyika na ligi nyengine Ulaya , ligi ya Premia ilikubali kufuata sera za serikali.
Lakini huku klabu kadhaa zikiathiriwa moja kwa moja na virusi hivyo, maadili ya ligi hiyo yapo katika mashakani. Ligi ya Premia na ile ya EFL zingependelea mechi zake zote zilizosalia kuendelea bila pingamizi yoyote.

 

 

Iwapo Euro 2020 itaahirishwa na Uefa kwa mwaka mmoja siku ya Jumanne huenda kukawa na fursa kwa mechi yoyote ilioahirishwa kuchezwa na huenda serikali ikaombwa kuahirisha mechi za ligi hiyo na EFL kwa wiki kadhaa.

 
Hatua hiyo itakabiliana na tishio la kushtakiwa na klabu ambazo huenda zikadai kwamba zimenyimwa fursa kushirikishwa katika mechi za kombe la Yuropa.

BBC

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments