Unamfahamu kwa sauti yake nyororo katika usomaji stadi wa habari, lakini je unafahamu kwamba kuna mengi kumhusu Tina Masika Mwana wa Ngema.
Swali langu la kwanza kwake nilitaka kujua kama amechukuliwa. Doh, kicheko alichotoa hapo, usiulize. ''limradi sijaolewa bado niko single''. Ndo lilikua
jibu lake. Najua mabachela wanafurahia kwa mtoto natural, wenyewe watakwambia. Mabinti wengi hupenda kujichubua kuweka nywele sijui makemikali , lakini Tina anasema hupenda sana kuweka nywele zake natural na itasalia hivyo.
Kwa sababu mtoto wa pwani basi ukitaka kumshika kwa urahisi, mpikie ugali na mkunde wa nnazi.
Mambo anayopenda kujishughulisha nayo asipokua kazini ? Kuogelea, kusoma vitabu, kutembea, ni baadhi tu .
Kwa picha hii, pengine utauliza ni mwanamitindo. Wala hasaha ni kujifurahisha tu.