priscillah

Mimi na watoto wangu tulikuwa tutolewe kama dhabihu – Priscillah

Bi Priscilla Obia mwenye umri wa miaka 28, ndiye alikuwa mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuaje.

Priscilla alifunga pingu za maisha na mumewe akiwa na miaka 21 na wawili hao amejaliwa na watoto wawili.

Kulingana naye amekuwa kwa ndoa ya migogoro na vita na anaamini mumewe alikuwa kwa dini la kishetani almaarufu cult.

Mwanamuziki maarufu nchini Uganda afariki baada ya kutekwa nyara, kuteswa

“Mara nyingi hapatikani nyumbani na kuna wakati fulani inabidi wakae pale kwa mikutano yao. Anaweza patikana siku moja kwa wiki na akija hukaa dakika kadhaa.”

Anasema mumewe hali chakula chake, isitoshe mambo ya chumbani ni kama amesahau.

Nilikuwa namuombea na siku moja mtu akaniambia mume wangu anapanga harusi mahali na kumuuliza akasema ako kwa cult na walimuambia asiwe na mimi mkristo kwani roho yangu haiambatani na maneno yao.

Alisema aliambiwa akisema atauliwa na hapo nilimuita na nikaita wahubiri wawili na alipofika alikiri kila kitu. 

Anasema kuwa mumewe akikutana na wale watu wanamfichia simu ili asizungumze naye na isitoshe kuna siku alipatikana akinitumia ujumbe na hapo walimchapa.

Pia anasema walimwambia kuwa hapaswi kufanya mapenzi nami na kuna wakati walimwambia alete picha yangu na mtoto aliye tumboni lakini hakuwapa kwani alifuta picha zote.

Wakazi wa Bungoma waishi kwa hofu baada ya kuvamiwa na chui

Kuna siku mzee wangu alinishikia kisu nikiwa na uja uzito na nilitaka niondoke usiku, nilitulia tu na nikagundua kuwa hata nikitoka mume wangu hangetambua.

Kuna siku bado akiwa mja mzito wimbo ulimjia kwa akili ukisema kuwa anapigwa vita mipakani mwake wimbo ambao ulikuwa unampa nguvu.

Priscilla anasema kuna siku sauti ya mwanadada akisema kuwa anapaswa atoke nje ili ajue mumewe ni kahaba, alipotoka alimwambia yule dada aingie kwa nyumba ili ampe uhondo wote.

Alisema yule mwandada alikuwa anatongozwa na mume wangu na anataka mtu ambaye hana mchezo kwani anatafuta mume. Isitoshe alikuwa na deni lake na hapo nikamlipa na akaondoka.

Mume wangu aliniambia kumbe yule mwanamke ni wa ile dhebehu yetu na kuwa ana nguvu kule lakini alipofika kwa mlango wetu nguvu zake zilimwishia.

Priscilla anasema kuwa wale watu walikuwa wanataka kumuua kupitia bwana yake ili wamtoe kama kafara. Mumewe alikuwa atupeleke out halafu kwa njia wasababishe ajali sisi tufe na watoto lakini yeye abaki.

Mzee yule naye alikuwa anunuliwe gari kwani damu yetu ndiyo ilikuwa ilipie ile nyumba.

Hata hivyo mungu aliwalinda na bado wako uhai na sahii wametengana.

Photo Credits: Stephen Manjala

Read More:

Comments

comments