Mimi ni bikra na sipo kwenye mahusiano na jinsia ya kike, Stivo Simple Boy

Screenshot_from_2019_12_12_09_37_35__1576132691_44882
Screenshot_from_2019_12_12_09_37_35__1576132691_44882
Msanii wa kizazi kipya Sitvo Simple Boy amesema kuwa bado hajafikia uamuzi wa kuwa na mwanamke katika maisha yake.

Stivo alitamba na ngoma ya Mihadarati na kujulikana katika tasnia ya muziki hapa nchini huku ngoma hii ikipata kuchezwa sana katika redio na runinga kuu nchini.

https://www.instagram.com/p/B5rwiJCF6Em/

Ngoma ya Mihadarati iliundwa katika maudhui ya kuwahamasisha vijana waepuke mtego wa dawa za kulevya.

https://www.instagram.com/p/B5R5y3flpeO/

Simple Boy alizua gumzo baada ya kusema kuwa hajawahi kuwa katika mahusiano na mwanamke yoyote katika mahojiano na chombo kimoja cha habari hapa nchini.

Msanii huyu amezaliwa na kukulia katika mtaa wa mabanda wa Kibra viunga vya jiji la Nairobi.

Aidha, Simple Boy amesema kuwa amedata sana na mrembo muigizaji wa filamu kutoka Tanzania anayefahamika kama Wema Sepetu.

Sepetu alikuwa mpenzi wa mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz.

Je, Unafikiri Stivo Simple Boy anaweza kupata nafasi ya kuvunja ubikira wake na staa wa Bongo Wema Sepetu?