'Mimi ni sharp shooter,' OtileBrown azungumzia mambo ya kitandani

Msanii Otile Brown akizungumza na msanii Juma Jux kwenye mitandao ya Instagram alimueleza jinsi yuko vyema kwenye sekta ya kitandani. Otile yuko tayari kutoa albamu mpya inayofahamika kama 'just in  love'.

Alisema kuwa yuko na ujasiri na yuko sawa kitandani. Alipoulizwa kama mpenzi wake Nabbi ni mjamzito alisema bado hana habari zozote.

"Unajuwa mimi ni sharp shooter, alisema kuwa ana habari njema za kuniambia lakini hajaniambia chochote unajua mimi ni sharp shooter." Alizungumza Otile.

Wakati walipoachana na Vera, alisema kuwa hamtimizii mahitaji yake ya kitandani huku akisema kuwa ana 'cassava' ndogo.

"Wakati ambao watu wametengana unahisi kila mmoja anapaswa kwenda njia zake lakini sanasana wanawake wanapenda kutangaza baada ya kutengana.

Lakini unapswa kusoma kutoka kwa mahusiano ambayo hayajafaulu."Alisema.

Baada ya kutengana na Vera Sidika alianza kumchumbia mpenzi wake Nabbi.