Mimi sijakataa kufika mbele ya kamati, Gavana Mutua ajitetea

mutua
mutua
Gavana wa Machakos Alfred Mutua ameishutumu kamati ya hesabu ya umma ya seneti na uwekezaji kwa kuandaa mikutano ya kisiri kwa malengo ya kumharibia jina.

Mutua ambaye aliandika katika mtandao wa Twitter siku ya jumanne alisema kwamba alijulisha kamati hiyo kuwa yuko mbali kidogo, lakini kamati hiyo bado lilimtaka afike mbele yao.

Kamati ya bunge ilimuelekeza Inspekta wa polisi Hillary Mutyambai kumkamata Mutua na kumfikisha mbele ya kamati hiyo ili ajibu maswali ya ukaguzi.

Kamati ya hesabu ya uhasibu na uwekezaji ya seneti ilitupilia mbali barua ya Gavana ikitoa sababu za kisisasa na kutoa sababu za kusafiri nje ya nchi.

Kamati hiyo iliomba nguvu zilizopewa na katiba na sheria ya nguvu ya bunge kutumia uwezo huo ili kumlazimisha mkuu wa kata afike mbele ya kamati hiyo.

Mutua alipuuza wito uliotolewa wiki chache zilizopita. Aidha alikuwa amepuuza mwaliko wa kamati ya kujitokeza mbele yake mnamo Septemba 18 kujibu hoja za ukaguzi wa miaka ya kifedha ya 2015-2016, 2016-2017, 2017-2018.