museveni

‘Mimi sio mgonjwa, ni uzani nimepunguza,’ Asema Museveni

Tovuti ya kibinafsi ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda iko chini baada ya kuchapisha chapisho lililoonyesha kuwa amekuwa akila chakula ambacho kimemsaidia kupunguza kilo 30kg.

Kwenye tovuti hiyo, alitupilia mbali uvumi wa afya mbaya au uchovu na akasema alipunguza uzani kwa mapenzi yake huku azma yake ikiwa kupunguza mafuta mwilini, tovuti ya habari ya Uganda ya soft Power inasema.

Wakati sababu ya tovuti yake kuwa chini haijulikani wazi, Soft Power ilichapisha tena, ikimnukuu Rais wa miaka 75 na kuandika:

Tovuti ya kibinafsi ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda iko chini baada ya kuchapisha chapisho lililoonyesha kuwa alikuwa akila chakula cha kumsaidia kupunguza kilo 30.

Wakati sababu ya blogi kuwa chini haijulikani wazi, Soft Power ilichapisha tena, ikimnukuu rais huyo wa miaka 75 kama kuandika: “Sina uchovu hata kidogo. Hata hivyo, nimepoteza uzito kwa kujitakia ili nipunguze mafuta niliyokubali yaongezeke mwilini mwangu kwa sababu madaktari walikuwa hawajatuelezea wazi kosa la kutopunguza mafuta. ”

Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, ameongeza kuwa sasa ana lengo la kuwa na uzani wake wa sasa wa kilo 76 kwa sababu unalingana na urefu wake wa 1.7m (5ft 7ins).

Photo Credits: The independent

Read More:

Comments

comments