Mimi siwezi kustahimili mahaba ya taabu! Vera Sidika Afunguka

NA NICKSON TOSI

Mwanasosholaiti Vera Sidika ameamua kubwaga manyanga siku chache to baada ya ripoti kujiri kuwa amewachana na mpenziwe kutoka Tanzania Jimmy Chansa miezi sita baada ya kuwa kwa uhusiano.

Kutokana na kisa hicho, pamekuwepo mabishano baina ya Vera na mfuasi wake kwa jina Halima kwa kile shabiki huyo amesema ni mwanadada huyo kuranda randa bila ya kukaa kwa uhusiano na mwanamume mmoja.

Halima aliandika hivi katika ukurasa wake;

"Twafahamu kuwa wewe ndio shida, si wanaume,"aliandika Halima.

Baada ya Vera kuona ujumbe huo, alionekana mwenye hamaki na kumjibu kwa kusema haya.

'

"Halima mimi siwezi kustahimili uhusiano ambao ni kama sumu eti ninajaribu kumfurahisha mtu, unaweza fikiri yale unayodhani lakini mwisho wa siku ni kuwa ni mimi nitafanya uamuzi wa maisha yangu. Kama unafurahishwa na hayo sema kwa sababu watu wamejaa kwenye mitandao kusema ya wengine ilhali yao imewashinda, sitawahi kuvumilia ujinga maishani mwangu mimi, nitachagua kilichokizuri kwangu na kibaya kukiachilia," alimjibu Vera.

Vera aidha hakuweza kufafanua iwapo mapenzi yake na Chansa na Otile Brown yalikuwa na shida zipi kwani alionekana  kana kwamba alikuwa kuzungumzia mahusiano hayo. Uhusiano wake na wawili hao ulidumu kwa takriban miezi 6 kila mmoja.

Mwaka 2017 Vera alitengana na mpenzi wake kutoka Nigeria kwa jina Yomi ambaye alikuwa amejongea kisima cha asali cha Vera kwa miaka 2 wengi wakadhani ya kwamba labda wangeoana lakini wakatengana .