Mipango kamili ya mazishi ya mcheshi Papa Shirandula yatangazwa

papa shirandula
papa shirandula
Mipango ya mazishi ya mcheshi Charles Bukeko almaarufu kama Papa Shirandula inaendelea huku mashabiki jamaa na marafiki zake wakiendelea kumuomboleza.

Papa aliaga dunia siku ya jumamosi 18/7/2020 baada ya kuugua kwa mda mchache.

Kulingana na jamaa zake, Papa aliaga baada ya kuugua ugonjwa wa Covid-19.

FFamilia yake imetangaza mipango ya mazishi yake

1. Mwili wake umetolewa katika hospitali ya Karen na sasa uko kwenye chumba cha kuhifadhi mauti cha Montezuma.

2. Mazishi yatafanyika jumatatu nyumbani kwake Busia.

3. Mipango ya usafiri tayari inaendelea ili waondoke Nairobi hii leo

4. Kesho watatangaza nambari ya Paybill ili wakenya waweze kuwasaidia kifedha. Kwa sasa kwa anayetaka kuchangia familia ya Papa anaweza kutumia nambari hii 0722102582.

Kulingana na shemeji yake Rorland Wanyama, Papa alikuwa amesafiri na aliporudi Nairobi aliugua na alipoelekea hospitalini hapo ndipo alipatikana na virusi vya Corona.

Familia yake iliamua kumtengea chumba chake nyumbani.

“Siku ya Jumapili hakuwa anahisi vyema baada ya kurudi Nairobi, hapo alielekea hospitalini katika hospitali ya Karen siku ya Jumatatu. Alipatikana na virusi vya Corona. Walikubaliana aelekee nyumbani ili akapewe huduma ya nyumbani. Hadi wa leo alipopata shida ya kupumua," Alisema.

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.