Mipango ya David The student kwa mamake kabla afariki (+ Picha)

Screenshot_from_2019_12_06_14_51_37__1575633127_90650
Screenshot_from_2019_12_06_14_51_37__1575633127_90650
David The Student almaarufu kama David Kangogo amesema kuwa alikuwa na mipango kibao kwa mamake mzazi.

David alikuwa na mipango ya kuhakikisha kuwa amemjengea mama nyumba pamoja na kumnunulia kijisehemu cha ardhi.

https://www.instagram.com/p/B5t2CtkAULc/

 "Ni mwezi tu ambapo nilimpigia dadangu nikimwambia mipango ya kununua kipande ya shamba ili nikujengee nyumba nzuri, kweli haya ni maisha," alisema David.

Katika ujumbe uliojawa na uchungu mwingi Insta, David amesema kuwa amekubali matokeo.

"Hakuna yeyote ambaye hujitayarisha kwa hiki kimetokea…nahisi kama ni ndoto niamke nipate ni ndoto hatari sana. Ila maisha kweli ni machungu…umesafiri kuishi na Mungu…" David The Student alichapisha.

 Wacheshi kama Sleepy David,MC Jessy, Carol Radull na wengineo wametuma pole zao.