Misa ya wafu ya Collymore kufanyaki kesho

Ibada ya ukumbusho ya Bob Collymore itafanyika hapo kesho katika kanisa la All Saints Cathedral.

Duka zote za Safaricom kote nchini zitasalia kufungwa kati ya saa nne unusu asubuhi hadi saa nane unusu mchana, kama heshima kwa marehemu.

Ibada hiyo ambayo itakuwa wazi kwa umma  itaanza mwendo wa saa tano asubuhi na itapeperushwa moja kwa moja kwenye runinga zote.

Collymore ambaye alikuwa afisa mkuu mtendaji wa Safaricom aliaga dunia Julai tarehe mosi nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 61.

Collymore alikuwa akiugua saratani na amemwacha mke na watoto wanne.

Mwli wa Collymore ulichomwa jana katika makaburi ya Kariokor katika hafla ya faragha iliyohuduhuriwa na familia na rafiki zake wa karibu.

Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Micheal Joseph amerejeshwa kuiziba nafasi ya Collymore kwa muda huku kampuni hiyo ikiendelea na shughuli ya kumtafuta afisa mkuu mpya wa kudumu.