Mistaken Identity? Mrembo katika sakata ya Willis Raburu na mkewe si mpenzi wa mtangazaji huyo, hata hamjui(Picha)

Willis Raburu t amejipata mitandaoni kwa sababu ambazo sio nzuri baada ya  Mpasho.co.ke kufichua kwamba ametengana na mkewe Marya Prude.

Iliripotiwa kwamba Raburu  na mkewe walikuwa wameachana na kila mmoja kuishi katika nyumba yake  baada ya mtangazaji huyo wa 10 over 10 kuwa na uhusiano wa pembeni.

Katika madai hayo, iliwekwa picha ya kipusa mmoja  mrembo kupindukia ambaye alidaiwa kuwa sasa ndiye anampa joto la usiku Raburu. Hata hivyo, inafichuka kwamba mrembo huyo ni mwathiriwa wa utumizi wa mitandao bila uthibitishaji wa maelezo na picha kwani  hata hamjui Raburu. Jina lake limetambuliwa katika instagram kama  Miva Noelle.

Sasa inabainika kwamba msichana huyo ni Mnyarwanda na sio Mganda kama ilivyokuwa ikidawa katika mitandao hapo awali

Picha za Edgar Obare katika mawasiliano naye zinaonyesha kwamba mrembo huyo amekuwa akisumbuka fikra baada ya rafiki zake kumtumia links zinazoonyesha picha yake ikitumiwa katika ripoti za madai ya kuwa mpenzi mpya wa Willis Raburu .

Raburu  na  Marya  wamekuwa na mwaka mgumu wa 2020 kwani baada ya kumpoteza mtoto wao kabla ya Marya kujifungua Januari tarehe moja, zimeibuka ripoti hizo kwamba wameachana .