Mitihani ya K.C.S.E na K.C.P.E ifanyike mwaka ujao- Sossion

Katibu mkuu wa kutetetea maslahi ya walimu nchini KNUT Wilson Sossion sasa anataka mitahani ya kitaifa ya kidato cha nne K.C.S.E  na ile ya darasa la nane K.C.P.E kufutiliwa mbali mwaka huu na kufanyika mwaka ujao 2021 kutokana na janga la corona ambalo limesitisha shughuli nyingi nchini.

Akihutubia wanahabari katika shirika la haki za kibinadamu lililoko katika mtaa wa Lavington, Sossion ameitaka serikali kuangazia namna itakavyojaribu kupunguza maambukizi ya virusi hivyo kabla ya kuangazia swala zima la K.C.S.E na K.C.P.E

Amesema ni sharti maisha ya walimu na wanafunzi yapewe kipaumbele kwanza na hatua ya kufungua shule haistahili kujadiliwa ama kuamuliwa kupitia njia ya kiimla.

“Resumption of schools must be a negotiable effort, not a dictatorship.” Amesema Sossion.

Sossion amesema ni heri wanafunzi kuendelea kukaa nyumbani ambapo wako salama kuliko wakiwa shuleni wakat nchi inapokabiliana na janga hilo.

“We would rather have all our children staying at home, safe and alive and repeating a year rather than sending them to school to die. The world will not come to an end if we suspend certain matters,” amesema Sossion.

Ameongezea kuwa mitihani ya kitaifa ya shule ya upili na ya msingi si tiketi ya kuingia mbinguni na inaweza kusongeshwa hadi walimu watakapomaliza kufunza silabasi.

“The national exams, KCPE and KCSE, are not a ticket to heaven. They can be postponed to suitable time when the syllabus shall have been covered and when the curve shall have been flattened.” Alisimulia Sossion.

Pia amewataka walimu walio na miaka zaidi ya 50 kusalia nyumbani akisema upo uwezekano mkubwa wa kuambukizwa virusi hivyo iwapo wataruhusiwa kufunza.

Ametilia mkazo swala la kumaliza silabasi akisema ni sharti shule zote zianze upya kufunza kwani si wanafunzi wote ambao wana uwezo wa kusomea kupitia dijitali.

Amepusilia mbali madai kuwa watahiniwa wa darasa la nane na kidato cha nne ni vyema kurejea shuleni ili kujianda kufanya mitahini. Akizungumzia swala hilo Sossion amesema ni heri kuokoa maisha ya watoto.

“We’ve heard of people talking about Form 4 and Class 8 reopening. These are human beings; the world will not come to an end. Children can repeat a class, better save lives first. Even if the exams are pushed to November 2021, if we can evade death, let’s do so.”

Ametaka pia serikali kutohitilafiana kivovyote vile na mishahara ya walimu wakati huu.

“Salaries of teachers must be protected. No one, whether government or private entities, should use Covid-19 to hold the salaries of teachers.” Sossion amesema