Mizani ya Haki,Naibu gavana wa Kilifi afikishwa kizimbani

NA NICKSON TOSI

Naibu gavana wa Kaunti ya Kilifi Gideon Saburi leo hii amefikisha mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili baada ya kukiuka amri ya serikali ya kujitenga kwa siki 14 baada ya kuwasili nchini akitokea Ujerumani.

Saburi alishikwa wiki jana na maafisaa kutoka kwa afisi ya mpelelezi mkuu waserikali  DCI na kukesha  ndani ya seli wikendi  hii iliyopita.

Saburi alipatikana kama ameambukizwa virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari na kulazwa katika hospitali kuu ya Mombasa.Hata hivyo,Waziri wa afya Mutahi Kagwe alipokuwa anatoa hotuba yake ya kila siku kwa taifa kuhusiana na Corona Alhamisi ,alisema kuwa Saburi atafunguliwa mashtaka kwa kwenda kinyume na amri ya Serkali.